Leo camera yetu ilitembelea bandari ya Bukoba na kukuta shughuli zikiendelea vizuri, na hali ya mazingira ikionekana katika hali ya usafi na kuvutia,viwanja vya bandari hiyo kwa sasa vimeboreshwa kwa kuwekewa sakafu ambayo imeondoa kabisa ile hali ya tope kipindi cha mvua na vumbi kipindi cha kiangazi,Lakini pia upo ujenzi wa mzani unaendelea 'mzani huu utakao kuwa ukipitisha gari iliyobeba mzigo na kuwezesha kutambua uzito wa mzigo kwa haraka zaidi. Pia camera yetu ilienda eneo la meli ya victoria ilipotia nanga,shughuli za upakiaji mzigo ulikuwa ukiendelea vizuri,.
Shughuli za upakiaji mizigo zikiendelea katika bandari ya bukoba mjini
Meli ya mv victoria ikiwa imetia nanga bandari ya bukoba,na shughuli za upakiaji mizigo zikiendelea
Wafanyabiashara wa ndizi wakishusha ndizi bandari ya bukoba kwa ajili ya kupelekwa Mwanza
Upakiaji mizigo melini hutumia craine ili kurahisisha upakiji kwa haraka na usalama zaidi wa mizigo na wabebaji mzigo
baharia shomari akiwa kazini
trector hutumika kuvuta tela la mizigo kusogeza eneo la kupakia
kapteni mwasa wa victoria (kushoto) akiwa katika mazingira ya bandari ya bukoba akiangalia shughuli zinavyoendelea
Kijana Bunduki akiwa na ndugu akida kwenye dirisha la tiketi
Dada Akida akiendelea na kazi zake
Ndizi mbivu zinazopelekwa mwanza kibiashara
Mama mjasiriamali akisubiri kupakia ndizi zake mbivu kupeleka Mwanza
Abiria wanaokwenda kwenda Mwanza wakikata tiketi dirishani
ndugu Methew Mathias(passenger Argent) bandari ya bukoba
Upimaji wa mizigo ukiendelea,mzani mkubwa unaojengwa kwa sasa utakapokamilika upimaji wa mizigo utakuwa rahisi zaidi
Eneo la bandari ya bukoba linavyoonekana,tope na vumbi kwa sasa ni historia.
Eneo la abiria kukaa na kusubiri kuingia melini limeboreshwa bandari ya bukoba
abiria wakisubiri muda wa kuingia melini kuelekea mwanza
Hapa ndio unajengwa mzani mkubwa bandari ya bukoba
MZANI HUU UKIKAMILIKA UTARAHISISHA UPAKIAJI WA MIZIGO KIRAHISI
ENEO LA GETI LA KUINGIA BANDARINI
TUNAIPONGEZA SERIKALI,WIZARA NA MAMLAKA YA BANDARI KWA KUBORESHA BANDARI YA BUKOBA ILI KUMUWEZESHA ABIRIA.MTEJA KUTUMIA HUDUMA ZA BANDARI YA BUKOBA. KWA HABARI ZA UHAKIKA ANGALIA jamcobk.blogspot.com
No comments:
Post a Comment