Thursday 16 May 2013

MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED BUKOBA WAFUNGA MTAA WA MIGEYO KUSHEREKEA UBINGWA!!!

Wadau mbalimbali na Mashabiki wa Machester United leo walijumuika Mtaa wa Migeyo ulipo Bukoba Mjini karibu na Soko kuu kushesherekea Ubingwa wa Man United ambao walikabidhiwa Mwali baada ya kuifunga Swansea City bao 2-1 siku ya jumapili iliyopita. Mbwembwe za mashabiki hao walijuika vizuri na kwa kuitana sehemu hiyo ya Mtaa wa Migeyo mnamo saa 6.30 mchana na pia kujumuika kupata Chakula cha mchana sehemu hiyo.
Upepo mzuri ukimpata shabiki huyu
Adui mwombee njaa...Gunners!!! Jezi ikikanyagwa baada ya Mashabiki kadhaa wa Gunners kuamia United na kuamua kuichukia timu hiyo ambayo inaukame wa makombe wa muda mrefu sasa na hata kwa msimu huu mpaka sasa kuona bado nafasi ya kuingia "Top 4" bado ni finyu sana, Ambapo wadau wanasema kuingia nafasi hiyo ni mpaka mechi za mwisho zitakazochezwa saa 12:00 na kuamua nani anaondoka na nani anaingia katika nafasi hiyo ili aweze kucheza ligi ya Mabingwa UCL.
Mjadala wa hatua ya mwisho ni ...
Ni kama kutaja rangi nyekundu ukimaanisha Man United, wadau wakionyesha wazi wazi na kwa kujiamini baada ya Timu yao waipendayo United Kuchukua ubingwa wa ligi kuu England.
Jezi hiyo tayari imeisha wekwa tayari kufanyiwa ambacho kilikuwa ni kama sheria yao kuitimiza!!
Kwa makini wadau wakiangalia kuhakikisha mambo yao yanakwenda kama yalivyopangwa.
Swali la kujiuliza lilikuwa ni je kwa nini Gunners!!!!??? kwa sababu ya ukame au!! maana wenzao Blues jana wamenyakua Mwali wao, City wamefanya mabadiliko ya kocha!! United nao wamefanya mambo yao safi!!

Kilichofata ni dawa ya moto ni moto!! kweli ukame utaisha kwa njia hii mhhh....

Na hii kaseme kwa Baba...
Mpaka majivu...

Wadau wa Manchester united wakifurahia


Kazi ya kuganga njaa ilifata..

Karibu....
Cha kuonesha kama ni Bukoba hakijifichi hapa...



Dadaz na Kaka walijumuika kwa pamoja kusherehekea Ubingwa wa Manchester United.

Karibuni sana jamani, ushindi mzuriiiiii...
Weka weka....kama Van Persie na goli...
Karibu ilifata...kwa wadau..
Kila mmoja alijipatia aina ya msosi aliotaka sehemu hiyo ambayo illitengwa kwa muda, ilikuwa ni sahani na kinywaji mkononi. kilichofata ni kusherekea ubingwa wa Mashetani wekundu
Muda wa punga uliendelea...
One love...hawa ni mayoso wa Mtaa wa Migeyo na hapa wanapunga mkono juu kama ishara ya upendo na peace ya ukweli kuungana na mashabiki wa Man United duniani kote...


United Daima!!!

No comments:

Post a Comment