Sunday 28 December 2014

LEO NDIO AROBAINI YA STIVIN LEORNARD MTENSA,WANAPAMOJA WATEMBELEA KABURI LAKE WAKIWA NA RAFIKI WA MAREHEMU BEN MULOKOZI

 MBAKUIGA BANYWANYI BAAWE MTENSA''''' Ni maneno mazito ya kihaya yenye maana kubwa(Wanakutafuta rafiki zako Mtensa) Ni leo majira ya saa tano asubuhi baadhi ya  Wanapamoja na Bw Ben Mulokozi wakiwa mbele ya kaburi la marehemu Mtensa nyumbani kwake alikozikwa siku arobaini zilizopita Kyakairabwa nje kidogo ya mji wa Bukoba, Nyuso za watu zikiwa na simanzi na majonzi ambazo imekuwa ngumu kusahau na kuwatoka sura ya Mtensa machoni mwao,Hali hiyo inajionyesha wazi kwa familia aliyoiacha mke wake , mama yake mzazi , watoto ndugu na jamaa tuliowakuta nyumbani hakika ukiwatazama wangali na majonzi makubwa na mpendwa wao Mtensa.
 Ni maeneo ya Lina's watu wakisubiriana kuelekea nyumbani kwa marehemu Mtensa.
 Kulia, ni Mwl Bube , watoto wake mapacha ambao wanaishi Sweden wamekuja likizo, jamco na Janiveva.
 Mh Matete akisalimiana na familia ya Mwl Bube.
 Hpoe Makoko akinena na wenzake.
 Nyumbani kwa marehemu.
 Mtu wa watu Ben Mulokozi akiwasili nyumbani kwa marehemu Mtensa,wakati wa mazishi hakuweza kuzika kutokana na kuwa nje ya nje,hivyo leo akatumia nafasi hii kuja kuhaani kwa familia.
 Mama Rubi nae akiwasil;i nyumbani kwa marehemu.
 Jack akimpokea  mgeni,, dada huyu JACK huwa ni mkarimu sana kwa watu  na hasa sambuli ya akina Ben Mulozi, asante Jack kwa ukarimu.
 Ben Mulokozi akisalimiana na watoto wa mwl Bube.

 Bw Pajero akiwa na mama rubi, hawa ni miongoni mwa watu waliopelekwa na marehemu Dubai kibiashara miaka ya zamani,wanamkumbuka kwa kuwaonyesha njia nyingi za kibiashara.
 Jerry akijaribu kuwachekesha wadau wasionekane wanyonge.

 Bw Wilson mchunguzi akiteta na familia ya Mwl Bube.
 Bw Ben Mulokozi akimpa mkono wa pole mama mzazi wa marehemu Mtensa.
 Mjane wa marehemu akikaribisha wageni.
 Mwenyekiti wa pamoja group Jamal Kalumuna akieleza kwa ufupi umuhimu wa siku ya leo ya kumkumbuka marehemu mtensa na kumuombea.
 Sala ikiendelea eneo la kaburi.
  Wa tatu kushoto ni Jeni veva alieongoza sala ya kumuombea marehemu.
 Mtensa tulikupenda sana, ila mungu amekupenda zaidi, tunakukumbuka sana daima na milele tutakuwa nawe kwa sala na kuenzi na kuyaendeleza mazuri yote.
 Mama mzazi wa marehemu hakika itamchukua muda sana kumsahau  mwanae ,maana kila ukikutana nae utadhani ndio msiba umeanza, mungu amtangulie.
 Rafiki mkubwa wa marehemu marehemu Mwl Bube akiongea kidogo kuhusiana na siku ya arobaini ya marehemu.
 Ta Folo wa pili kulia akisikiliza kwa makini.
Ni mtoto wa kiume mkubwa wa marehemu Stalonly akitoa shukrani wa wageni waliofika na kumuombea sala marehemu Mtensa.Pumzika kwa amani marehemu Mtensa tutakuklumbuka daima.

No comments:

Post a Comment