Wednesday 31 December 2014

AJALI MBAYA YATOKEA MAENEO YA ROUND ABOUT YA RWAMISHENYE JIONI HII.

 Ni Lori la kubeba vifusi ambalo lilitambulika kumilikiwa na kampuni inayochimba visima vya maji na kutengeneza mtandao wa mabomba ya maji Manispaa ya Bukoba leo jioni liliacha njia maeneo ya mzunguko wa Rwamishenye, njia ya kuelekea Mutukula,Kwa mujibu wa maelezo ya walioshuhudia inasemekana Lori hilo inawezekana lilikatika breki likiwa limepakia kifusi cha udongo,Hata hivyo inasemekana dereva wa gari hili alionekana amelewa na kupelekea kushindwa kumudu kuendesha gari hilo. Hakuna aliepoteza maisha.

Huyu ndio inasemekana alikuwa dereva wa lori lililopata ajari , na inasemekana alikuwa amelewa kwa mujibu ya watu walioshuhudia tukio.Alipambana na askari wa usalama barabarani akigoma kupanda gari ya polisi akidai yeye si dereva wa hilo gari, baada ya kupambana polisi walifanikiwa kumzibi na kumpeleka kituoni.

No comments:

Post a Comment