Wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Runazi Kanyanyamiongo wilayani Muleba wamevamia nyumba mbili na kuzibomoa na mojawapo kuichoma moto na kufyeka shamba la migomba kwa kuwatuhumu wenye mali hizo kuwa ni majambazi. Nikiongea na mmoja wa mkazi wa kijiji hicho aliejitambulisha kwa jina moja la Yahaya kuwa Bw Masanja Buyunge aliebomolewa nyumba na kuchomwa ni mfugaji anaemiliki ng'ombe zaidi ya miambili na rafiki yake Mwandikilo Makimu aliebomolewa nyumba na kufyekewa migomba yote na mabati kutobolewa wanashukiwa kuwa ni majambazi na walimnyang'anya kijana mmoja pikipiki yake na wamekuwa wakishukiwa kwa muda mrefu na wanakijiji kuwa ni majambazi na hivyo kusababisha kuchukuliwa hatua ya kubomolewa nyumba zao na mifugo yao kuchukuliwa na baadhi ya wananchi wenye hasira kali.
Hii ni nyumba ya Bw Mwandikilo Makimu iliyobomolewa na wananchi wenye hasira kali
Shamba la migomba likiwa limefyekwa
Badhi ya wananchi waliokuwa safarini kuelekea Mwaza wakipata maelezo kutoka kwa wenyeji
Wananchi wenye hasira kali baada ya kubomoa nyumba na kufyeka migomba kilichofuatia walitoa Ngombe kwenye zizi la mtuhumiwa na kumchinja na kila aliekuwepo akapata nyama,na baadhi ya ng'ombe walitoka zizini na kusambaa maeneo tofauti
Mmiliki ya jamcobukoba.blogspot akiwa katika eneo la tukio akiwa safarini kuelekea Mwanza akakutana na kisanga hiki
Bw Bushira nae akishuhudia tukio
Ni baadhi ya mifugo iliyookolewa ya watuhumiwa ujambazi,polisi wameweka ulinzi wakati swala hili likifanyiwa uchunguzi
Hii ilibomolewa na kutiwa moto
Mwenye koti jeusi ni Bw Amasha ambae anaishi eneo lilipotokea kisanga akielezea
Wadau walikuwa safarini wakakutana na majanga haya
MAMA HUYU NA WANAE WAWILI Ni mke wa mtuhumiwa Masanja Buyunge aleleza kua majira ya saa kumi usiku lilikuja kundi kubwa la watu na kuwaamuru wafungue mlango, na walipoingia ndani walimuhitaji mme wake wakamtoa na kuwamuru watoke ndani na kuanza uharibifu wa kubomoa nyumba na kuchoma moto.
Wakati tukiondoka eneo la tukio vyombo vya usalama vilifika na wapo katika uchunguzi
Mimi na wewe hatujui ukweli ukoje,je wananchi ni halali kujichukulia sheria mkononi,je ni halali kuchinja mifugo na kuchukua nyama,yote hayo tusubiri mwisho wake
No comments:
Post a Comment