Friday 23 May 2014

KIKAO CHA WADAU WA HAKI JINAI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KAGERA CHAFANA LEO TAR.23/05/2014

Mgeni rasmi Mh. Jaji Pelagia Khaday(katikati) Wakili wa Serikali Mfawidhi Bi. Sakina Sinda (kushoto) na kulia ni Mkuu wa Upelelezi wa Jinai Mkoa Kagera Bw. Henry Mwaibambe (ACP).Mgeni rasmi Mh. Jaji Pelagia Khaday(kulia) na kushoto ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Bi. Sakina Sinda.
Wajumbe wakisikiliza kwa makini mada inayotelewa
Taswira Wajumbe

Wajumbe na wadau wa Haki Jinai wakifuatilia majarida
Na Faustine Ruta, Bukoba
Kikao cha Wadau wa Haki Jinai kimefanyika leo Ijumaa Asubuhi na Kikao hicho Kimejumuisha Mawakili wa Serikali, Mkuu wa Upelelezi wa Jinai Mkoa na Wakuu upelelezi Wilaya, Mganga Mkuu wa Mkoa, Waganga kutoka Wilayani, Walinzi wa Amani(Afisa watendaji) na Mdau Mwalikwa Mhazini wa Hazina ndogo Bukoba.Kikao hiki kikiwa na Malengo yanayotokana na Uhiari wao wa kutekeleza Miongozo, Kanuni na Maelekezo Mbalimbali ya Viongozi.
Kikao hicho kikiwa ni Muhimu kwani walijadili Changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kazi zao za Upelelezi na uendeshaji wa Mashtaka katika Mahakama zao hapa Mkoani Kagera. Katika Kikao hicho pia wamekumbushana na kuhamasishana kuzingatia Misingi ya Haki za Binadamu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa Vile Utekelezaji wa majukumu moja kwa moja Unahusisha tuhuma na Malalamiko toka kwa Wanajamii.
Kikao hicho pia kimesukumwa na Hali halisi waliyonayo ya Takwimu za Mshauri ya Jiani ya Muda Mrefu yaliyopo Mahakamani na kuonelea kwamba ipo haja kwa wao Wadau Mkoa wa Kagera kukaa Pamoja na kujadili Changamoto hiyo na kuweza kupitia Ufumbuzi wa kuweza kwenda sambamba na Kauli Mbiu ya siku ya Sheria Nchini isemayo "UTENDAJI HAKI KWA WAKATI, UMUHIMU WA WASHIRIKI WA WADAU". Kujadili jinsi ya kushughulikia tuhuma na mshauri dhidi ya Watoto. Kubadilishana Uzoefu wa Jinsi ya kuyashughulikia Mashauri ya Watoto.




Wakili wa Serikali Mfawidhi Bi. Sakina Sinda akitambulisha Baadhi wa Wageni
Mgeni rasmi Mh. Jaji Pelagia Khaday akitoa Hotuba yake

Wakili wa Serikali Mwandamizi Bi. Jaqueline E. Mrema akitoa Mada yake kuhusu Changamoto zitokanazo na Upelelezi katika uendeshaji Mashtaka ya Jinai.
Mkuu wa Upelelezi wa Jinai Mkoa Kagera Bw. Henry Mwaibambe (ACP) na Wakili wa Serikali Mfawidhi Bi. Sakina Sinda wakimsikiliza kwa makini Wakili wa Serikali Mwandamizi Bi. Jaqueline E. Mrema wakati anatoa Mada.

Kwa makini wakisikiliza Mada
Mkuu wa Upelelezi wa Jinai Mkoa Kagera Bw. Henry Mwaibambe (ACP) Akitoa Mada yake kuhusu Masuala muhimu ya Upelelezi.
Taswira ya Wajumbe na Wadau kwenye Ukumbi wa Jengo la NCCF hapa Mjini Bukoba kwenye kikao cha Wadau wa Haki Jinai.



Mpiga picha Bw. Samwel Mitema wa Offisi ya RCO Kagera akichukua kumbukumbu live kwenye kikao

Picha ya Pamoja
Picha za Pamoja Viongozi wakuu na wajumbe

Mawakili wa Serikali pamoja na Viongozi wakuu.


Kulia ni Dada Pili Kilo anayefuata ni Alphonce John










No comments:

Post a Comment