Tuesday 11 February 2014

KAMATI KUU YA CCM YAMTEUA MTOTO WA MAREHEMU MGIMWA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) akimtambulisha kwa waandishi wa habari, mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Mkoa wa Iringa, Godfrey William Mgimwa (kushoto), wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, baada ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM. 

Nape amemtambulisha Godfrey ambaye ni mtoto wa Marehemu Dk. William Mgimwa, baada ya Kamati Kuu ya CCM leo kumpitisha kuwania nafasi hiyo ya Ubunge.

No comments:

Post a Comment