Tuesday, 11 February 2014

JENGO LA GHOROFA 18 KARIBU NA IKULU DAR KUPUNGUZWA

Jengo lenye ghorofa 18, lililo karibu na Ikulu linalotakiwa kupunguzwa kuanzia ghrifa ya saba kwenda juu.

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu, Richard Maliyaga, kila mmoja kulipa faini ya Sh. Milioni 15 au kwenda jela miaka tisa baada ya kuwatia hatiani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuruhusu ujenzi wa jengo la ghorofa 18 karibu na Ikulu.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo alisema jengo hilo lilipaswa kuwa la ghorofa sita na kuamuru kubomolewa kuanzia ghorofa ya saba kwenda juu.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai jana alitoa hukumu ya kupunguzwa kwa baadhi ya ghorofa kadhaa ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya hukumu hiyo yenye kifungu cha 40, namba 1 na 2 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ambacho kinawaruhusu kutaifisha jengo hilo.

No comments:

Post a Comment