Thursday, 23 May 2013

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI TUMAINI MANISPAA YA BUKOBA WAKO HATARINI KUPATA MAGONJWA YA MILIPUKO,IKIWA NI MOJA WAPO YA CHANGAMOTO YA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA

 wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Tumaini manispaa ya bukoba wako hatarini kupata magonjwa ya milipuko kutoka na wapita njia kutumia  vyoo vya shule kutokana na ukosefu wa uzio katika shule hiyo,Akiongea kwa masikitiko mwalimu mkuu wa shule hiyo Tegamaisho Deogratias alisema wakazi wengi wanaoishi kashai ukatiza katika maeneo ya shule ,na wengi wao hutumia vyoo vya shule,bwana tegamaisho aliendelea kusema kuwa baadhi ya wazazi wameleta malalamiko kuhusu watoto wao ambao wamekutwa na tatizo la UTI,kingali ni watoto wadogo.
 changamoto nyingine waliyonayo ni uchakavu wa miundo mbinu,mwalimu tegamaisho amesema wakati wakifidia kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege walipewa kiasi cha shilingi laki sita kwa ajili ya miti na mazao yaliyokuwa katika eneo hilo, lakini uharibifu wa miundo mbinu na majengo uliotokea katika shule hiyo hawakuwahi kulipwa chochote, kitu ambacho kimesababisha wanafunzi kusoma katika mazingira magumu sana,amesema shule hiyo imeezekwa na mabati ya udongo(vigae) amayo ni ya miaka mingi sana ambayo yameishatoboka na kipindi cha mvua wanafunzi wanalazimika kusogeza madawati  maeneo ambayo hayavuji.


 mwalimu mkuu amesema ukosefu wa uzio katika shule hiyo mbali ya usalama wa afya'pia swala la wizi wa vifaa vya shule kutokana na watu wengi kupita katika maeneo ya shule





                                                                         mambo ya ngoma hayo.......
                                   mstalini.... wengi wenu haya maisha mmepitia kufikia hapo ulipo

                                                                mwalimu akisisitiza jambo kwa wanafunzi


Itakumbukwa tarehe 31 08-1994 wanafunzi wanne wa shule ya msingi tumaini walipoteza maisha kutoka na bomu la mkono kulipuka hapo shuleni,pia wapo wanafunzi waliopata ulemavu wa kudumu,swali linakuja shule hii ambayo inachangamoto nyingi kutokana na upanuzi wa uwanja wa ndege,shule ambayo naweza kusema iko katika njia ya ndege ikiwa angani, usalama wake ukoje? walisema wataalamu wa lugha TAHADHALI KABLA YA HATARI..... YETU NI HAYO KWA LEO.

No comments:

Post a Comment