Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameandaa
futari leo (Julai 17 mwaka huu) kwa wadau mbalimbali wa mpira wa miguu.
Shughuli hiyo itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo waalikwa wataanza kuwasili saa 11.30 jioni.
Waalikwa
katika futari hiyo wametoka katika makundi mbalimbali. Makundi hayo ni
wadhamini, klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza za Dar es Salaam ambazo
zitawakilishwa na watu wawili wawili.
Viongozi
wa zamani wa TFF, Said El Maamry, Leodegar Tenga, Muhidin Ndolanga,
Athuman Nyamlani, Mwina Kaduguda, Michael Wambura, Fredrick Mwakalebela
na Ashery Gasabile. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF waliopo Dar es
Salaam, Wizara ya Michezo na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Vyama
shiriki; TWFA, TAFCA, TASMA, SPUTANZA, FRAT ambavyo vitawakilishwa na
watu watatu watatu, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA), Baraza la Michezo la Taifa (BMT), wahariri wa habari za
michezo, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na
Polisi kanda Maalumu- Dar es Salaam.
Wajumbe
wa kamati ndogondogo za TFF waliopo Dar es Salaam, wazee wa Simba na
Yanga- watano kutoka kila klabu, timu ya Serengeti Boys, klabu ya
Saigon, Bodi ya Ligi Kuu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wakuu wa wilaya
za Dar es Salaam, wabunge wa Dar es Salaam, Meya wa Dar es Salaam, Meya
wa Kinondoni, Meya wa Ilala na Meya wa Temeke.
Waalikwa
wengine ni Omari Abdulkadir, Amin Bakhresa, Harudiki Kabunju, Hamis
Kissiwa, Ismail Aden Rage, Masoud Sanani, Jamal Bayser, Hassan Dalali,
Imani Madega na Mbaraka Igangula.
No comments:
Post a Comment