Thursday 17 July 2014

JOSIAH GIRL'S HIGH SCHOOL YAPASUA KIMKOA NA KITAIFA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA

 Katika picha ni baadhi ya wanafunzi waliohitimu  kidato cha sita wa Josiah girl's high school .Katika hali ya kuonyesha mafanikio makubwa ya shule katika taaluma wanafunzi wote wamefauru na kupata daraja la kwanza na kupelekea shule kuongoza katika nafasi ya 1 kimkoa kati ya shule 11,Kitaifa imekuwa 1 kati ya shule 180. katika ufauru wa kila somo kitaifa Josiah Girl's High School General Studies imekuwa 63 kati ya shule 448 kitaifa, somo la History imekuwa ya  9 kati ya shule 406, somo la Geography imekuwa 1 kati ya shule 431, na English Language imekuwa 3 kati ya 380. Shule ya Josiah Girl's High School ipo katika Manispaa ya Bukoba kata  ya Ijuganyondo kilometa sita kutoka mjini,ipo eneo zuri na mazingira mazuri ya kumfanya mwanafunzi aweze kusoma vizuri, wanao walimu wenye uwezo  wa kufundisha,shule  inaanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita.
 Picha kutoka maktaba yetu Mkuu wa shule katika mmoja ya matukio shule hapo
 Baadhi ya timu ya walimu
 Josiah Girl's ni miongoni mwa shule chache nchini ambao wanajifunza masomo yao kwa kutumia tablets
 Wananawake wananaweza asikudanganye mtu..


No comments:

Post a Comment