Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Leonidas Gama akimpokea Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tarehe
28.4.2014. Mama Salma alikwenda Moshi kuzindua rasmi chanjo ya kuzuia
maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wa umri wa
miaka 9 hadi 16.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma
Kikwete akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia watoto,
UNICEF, hapa nchini Dkt. Sudha Sharma, mara baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa Mandela uliopo katika eneo la Pasua katika Manispaa ya Moshi
kwa kulikofanyika uzinduzi rasmi ya chanjo ya saratani ya shingo ya
kizazi kwa wasichana.
Maandamano
ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita mbale
ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa
chanjo kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi tarehe 28.4.2014.
Maandamano
ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita mbale
ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa
chanjo kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi tarehe 28.4.2014.
Mamia
ya watu waliohudhuria sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia
maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wakifuatilia
kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete katika sherehe
hiyo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi na wanafunzi
waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia saratani ya
shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 16 huko Pasua,
Moshi tarehe 28.4.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa
wasichana kwenye sherehe iliyofanyika huko Pasua, Moshi Mjini tarehe
28.4.2014. Wengine katika picha (kushoto kwenda kulia) ni Ndugu Leonidas
Gama, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Rufaro Chatora, Mwakilishi wa
Shirika la Afya Duniani hapa nchini, Dkt Kebwe Stephen Kebwe, Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila, Mkurugenzi
wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Mama Salma na wa Kwanza kulia ni
Mwakilishin wa Shirika la Kuhudumia watoto (UNICEF) hapa nchini Dkt.
Sudha Sharma.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza naza mtoto Salma Abillah mara
baada ya kupata chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi na baadaye
kumkabidhi kadi yake ambayo anatakiwa kurudi tarehe 28.10.2014 kwa
ajili ya kupata chanjo ya pili.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana akitoa chanjo ya matone kuzuia
ugonjwa wa polio kwa mtoto Ahmad, miezi 10, aliyefika kwenye sherehe ya
uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi
kwa wasichana huko Pasua, Moshi
No comments:
Post a Comment