Dar es Salaam.
Watanzania wawili
wanashikiliwa nchini Misri baada ya kukamatwa wakiwa na kilo saba za
dawa za kulevya aina ya heroin wiki mbili zilizopita walizokuwa
wameficha kwenye begi la nguo.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi jana Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Wizara ya Mambo ya Nje
na Uhusiano wa Kimataifa, Mkubwa Ali, alikiri kukamatwa kwa watu hao
(majina yanahifadhiwa) ambao mmoja ni mkazi wa Ilala na mwingine wa
Magomeni jijini Dar es Salaam. “Taarifa tulizonazo zilizo rasmi kutoka
Ubalozi wa Tanzania nchini Misri kwa sasa ni kukamatwa kwa Watanzania
wawili waliokuwa wakisafirisha heroin kuelekea Bara la Asia na
walikamatwa nchini Misri wiki mbili zilizopita.”
“Tumewasiliana na balozi wetu
nchini Misri amesema hana taarifa za kuhukumiwa kunyongwa kwa watuhumiwa
hao, isipokuwa wameshasomewa shtaka lao la awali. Wapo rumande kwa sasa
kwani kesi hiyo imetajwa mara moja tu. Balozi amekiri kushikiliwa kwa
watuhumiwa hao wakiwa na dawa zinazoaminiwa ni za kulevya,” alisema.
Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa polisi na wanatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote.
Video inayomwonyesha mmoja
akikaguliwa na maofisa wa polisi wa nchini Misri na kukutwa na dawa
hizo, ilisambaa siku nne zilizopita katika mitandao mbalimbali ya
kijamii.
Kwa mujibu wa sheria za Misri
kama ilivyo kwa nchi za Bara la Asia, mtu akikamatwa na dawa za kulevya
hukumu yake ni kunyongwa hadi kufa. Kutokana na sheria za nchi hiyo,
tangu kukamatwa na Watanzania habari zimeenea kuwa huenda wakanyongwa.
Habari za uhakika kutoka kwa
ndugu wa karibu wa mtuhumiwa huyo, zilidai kuwa walikuwa hawafahamu kuwa
alikuwa anajihusisha na dawa za kulevya.
“Huyu ni ndugu yangu kabisa lakini nilikuwa sijui kama anafanya mambo kama hayo’’ alisema.
Kama atanyongwa ni pigo kubwa kwetu,” alisema mmoja wa ndugu wa Sharifa ambaye hakupenda kutaja jina lake.
Alisema miaka mitatu iliyopita
ndugu yao wa kike mwenye mtoto mmoja alikuwa akifanya kazi katika
Shirika la Nivea na alikuwa hana tabia mbaya.
Mthumiwa mmoja wapo akiwa na mwanae wa kike |
Jana mwandishi wa habari hizi
alilifika katika Ubalozi wa Misri nchini ili kufahamu kwa kina habari
hizo, ambapo balozi wa nchi hiyo hakuweza kuzungumzia lolote.
Hapa
chini kuna link ambayo iko uptodate inforamtion ya adhabu ambazo
wathumiwa mbali mbali hupata nchini Egypt baada ya kuhukumiwa na case
tofauti ikiwemo madawa ya kulevya bofya ujisomee.
Death Penalty WorldWide
No comments:
Post a Comment