Katika secta ya afya nchini imekuwepo changamoto kubwa kuhusiana na uhaba mkubwa wa huduma za afya kwa kutokuwa na Mahospitali sambamba na wataalamu,na kusababisha tatizo kubwa katika jamii kubwa ya Tanzania,Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha inatatua tatizo hili ikiwa ni pamoja na kushawishi Taasisi,Mashirika na watu binafsi kuanzisha na kufungua Mahospital na zahanati katika kukabiriana na tatizo hili. Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la COSAD lililopo Marekani,Tanzania na wadau wengine nchini Canada Bw Smart Baitan aliliona hilo na kudhamili kwa dhati kuhakikisha anakuwa miongoni mwa watu wachache wazalendo wanaokumbuka na kusaidia watu katika jamii wenye uhutaji wa mambo mbalimbali sambamba na huduma za afya. Na sasa anaandika historia Tanzania, Mkoa wa Kagera Manispaa ya Bukoba , Waziri wa maliasili na Utalii Mh Lazaro Nyalandu anafungua rasmi zahanati ya Cosad(COSAD CLINIC) yenye ubora wa vifaa vya kisasa na wataalam waliobobea katika nyanja ya afya chini ya Dr Jessica Baitan.
Mh Nyalandu akiwa na meneja wa uwanja wa Bukoba akimkaribisha
Bw Smart akimpa ratiba waziri ya shughuri nzima
Mc wa shughuri nzima Bw Kimu akiendelea na utaratibu
Dr Jessica Baitan akiwa na Dr Pamera kutoka wizara ya afya
Watu wakiwa kazini
Mwenyekiti wa wasanii kanda ya ziwa Anitha Zihimbile
Kikundi cha ngoma kutoka Ngara
Mchungaji Ben Swanson kutoka Marekani akitoa neno.
Tumetoka mbali mh dah...... unakumbuka hizi zile kule shule.duh acha mungu aitwe munguuu
Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu akitoa neno,ametoa wito kwa watanzani wanaohishi nje ya nchi kuwa wazalendo na waige alichokifanya Smart Baitan kuleta maendeleo Nyumbani.
Pamoja na kutoa huduma ya kubeba wagojwa katika jimbo la Balozi Kagasheki , na majimbo mengine Balozi kagasheki kwa kutambua mchango mkubwa uliotolewa na Cosad amesema Gari hili litakuwa likitoa huduma pia katika zahanati ya Cosad na ametoa nyumba kwa ajiri ya wataalamu mbalimbali watakokuja kusaidia wagonjwa kuishi bure.
Uzinduzi rasmi wa zahanati ya COSAD
JAMCO uliipamba COSAD 2014. Maoni??
ReplyDelete