Saturday 4 October 2014

UFUNGUZI WA MAKAO MAKUU YA COSAD BUKOBA,BALOZI KAGASHEKI AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WAFADHIRI WANAPOLETA MISAADA KUSAIDIA JAMII

 Hakika miongoni mwa watu ambao ni vigumu sana kuisahau tarehe 3-10-2014 ni Mkurugenzi Mtendaji wa COSAD nchini Tanzania Ndugu Smart Baitani kwani ndoto yake imetimia ya ufunguzi wa miradi ya kusaidia jamii ya Bukoba na Wananchi wote kwa ujumla.
 Ndugu Smart Baitan akiteta na Balozi Kagasheki nyumbani kwake ambapo aliukaribisha ugeni wa Cosad kupata kifungua kinywa kabla ya shughuri ya uzinduzi wa miradi kuanza.
 Wageni wakipata chai kwa Balozi Kagasheki
 Bi Anitha Zimbihile akiwa na Bw Almasoud Kalumuna Mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa wa ccm.
 Bw Ramadhani Kambuga Mwenezi wa ccm Manispa
 a ya Bukoba akisalimiana na Bi Anitha  mwenyekiti wa wasanii kanda ya Ziwa
 Baba Askofu Methodius Kilain akiwasili Makao Makuu ya Cosad
 Kulia ni Bw Cladius Mutabuzi msanii maarufu katika bendi ya Kakau.

 Wageni waalikwa
 Muonekano wa Matent
 Ni kwaya iliyotoka wilayani Ngara wanafamilia wa Cosad wakitoa burudani na kutoa ujumbe mzito kwa kushukuru uzinduzi wa miradi ya Cosad
 Bw Smart Baitan akiwa na mkewe Dr Jessica Baitan
 Wafanyakazi wa Cosad
 Bw Smart Baitan akitoa maelezo kuhusiana na Cosad
 Bw Baitan akitambulisha wafanyakazi wa Cosad
 Mc wa shughuri nzima Harris akiendelea kuchombeza
 Embutuu, moja ya ngoma maarufu nchini Uganda
 Mh Diwani Mwajabu Galiatano
 Kulia mmoja wa marafiki wa bw Baitan anaehishi nje ya nchi amekuja kushuhudia tukio la kihistoria la Cosad
 Mgeni Rasmi akitoa hotuba yake kabla ya ufunguzi,amekemea baathi ya viongozi ambao wamekuwa wakikwamisha jitihada za kusaidia jamii.
 Wanafamilia wa Cosad kutoka Muleba
 Balozi Kagasheki akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Makao makuu ya Cosad Bukoba, Awali Balozi Kagasheki alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji Bw Smart Baitan kwa jitihada zake za muda mrefu kuhakikisha analeta miradi ya kusaidia jamii Bukoba na hususani kwenye jimbo lake, ndipo alipotoa wito kwa jamii na hasa viongozi wa serikali kuwapa mosemyo na kuthamini jitihada za watu kama Baitan wanaojari na kuthamini kuleta maendeleo ya kusaidi jamii. Balozi Kagasheki aliendelea kusema inasikitisha sana kuona baadhi ya viongozi wenye dhamana serikalini wamekuwa wasumbufu na kukatisha tamaa watu wanaojitolea kusaidia jamii kwa kujifanya miungu watu wanapokuwa katika nafasi zao za kaza na kupunguza kasi ya maendelea.Katika kuonyesha jinsi alivyoguswa na miradi na hasa mradi wa zahanati utakaojari mama na mtoto amejitolea nyumba kubwa ya kisasa kwa ajiri ya matumizi mbalimbali kwa shirika la Cosad, Pia amewaeleza kuwa katika ofisi yake lipo Gari la kubeba wagonjwa wanaweza kulitumia wakati wowote watakapolihitaji,Ametoa wito kwa watu wote kuwa na moyo wa kusaidia jamii na kumtaja Baba Askofu Methodius Kilain kuwa pamoja na kazi ya mungu aliyonayo, lakini pia amekuwa mstari wa mbele katika harakati za ushawishi wa kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.







 Baba Askof Kilain akiangalia mitambo mbalimbali iliyomo katika studio za kurekodi kazi za wasanii
 Mapokezi ya msaidizi wa Balozi wa Marekani ncini Tanzania Bw Vicent Spera uwanja wa ndege wa Bukoba ambae amekuja kwenye ufunguzi wa miradi ya Cosad
 Blogger wa Bukobawadau sambamba na msaidizi wa Balozi wa Marekani
 Cosad Center
 Kundi kutoka Uganda likiburudisha
 Hapana chezeaa Cosad
Ilikuwa ni furaha tupu

1 comment: