Thursday, 2 October 2014

HATIMAE COSAD KUANDIKA HISTORIA MPYA MANISPAA YA BUKOBA,BALOZI KAGASHEKI ATEMBELEA MIRADI KABLA YA UFUNGUZI RASMI 3-10-2014 IJUMAA

 Wahenga walisema kawia ufike na wengine husema mambo mazuri hayataki haraka, yamedhihirishwa na Cosad baada ya ndoto yao ya muda mrefu ya kuweka miradi mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba kwa ajiri ya Jamii kupata huduma na kujikwamua katika wimbi la umasikini uliokithiri kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi nchini.Cosad  ni shirika lisilo la serikali Tanzania wanaweka histori mpya ya kufungua miradi katika upande wa afya kwa kufungua Zahanati katika kata ya Kashai maeneo ya Nyamkazi,Shamba la Mbuzi wa maziwa  kata ya kagondo,Studio ya kurekodi kazi za wasanii(Imuka Recording Studio),Kituo cha Teknolojia na Biashara na Ofisi mpya za makao makuu ya Cosad Nchini.Katika picha ni Uongozi wa Cosad ukimpokea Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki katika uwanja wa ndege Bukoba na badae kutembelea maeneo yote ya Miradi kabla ya ufunguzi rasmi 3-10-2014.
 Balozi Kagasheki akipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji  wa Cosad Tanzania Bw Smart  Baitan
 Dr Susan McCormick Hadley akisalimiana na Balozi Kagasheki uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Hili ndio jengo la  Zahanati itakayofunguliwa maeneo ya Nyamkazi Bukoba
 Bw Smart akitoa maelezo kuhusiana na mradi wa Zahanati  Kwa Mh Mbunge
Kulia mmoja wa wajumbe wa bodi ya Cosad anaehishi Marekani akiwa na wafanyakazi wa Casad Tanzania.
 Eneo la Mapokezi
 Baadhi ya vifaa vya kisasa vitakavyotumika
 Balozi Kagasheki baada ya kuona alikubali na kushukuru kazi kubwa iliyofanywa na Cosad jimboni kwake
 Maeneo ya kupumzisha wagojwa
 Balozi Kagasheki na mmoja wa waandishi na mtangazaji wa Clouds Redio na TV
 Ofisi za Cosad maeneo ya Kashura mlimani.
 Eneo la Mapokezi
 Eneo la mikutano na Mazungumzo
 Eneo la Studio kwa ajiri ya kurekodi kazi za wasanii
 Uongozi wa Cosad wakiwa nyumbani kwa Balozi Kagasheki Maeneo ya Kitendaguro kwa mapumziko mafupi .
 Picha ya pamoja nje ya Nyumba ya Balozi Kagasheki
 Hapa ni Kituo cha Teknologia na Biashara cha Cosad kilichoko Kata ya Kibeta Bukoba Manispaa
 Balozi Kagasheki akisalimiana na Mtoto wa Bw Smart Baitan
 Dr Jessica  Baitan akisalimiana na Balozi  Kagasheki
 Eneo la ndani Kituo cha Teknolojia na Biashara cha Cosad
 Mtoto mdogo wa Bw Smart Baitan.
 Mradi wa mbuzi wa maziwa

 Mbuzi wa maziwa
 Balozi Kagasheki akipewa maelezo jinsi wakina mama wanavyonufaika na mradi huu
 Kushoto ni  kijana anaehudumia mbuzi
 Balozi Kagasheki Live Cloud's Redio akieleza kile alichokiona katika ukaguzi wa miradi itakayofunguliwa rasmi 3-10-2014 jimboni kwake
 Baba ASKOFU Bagonza mmoja wa wajumbe wa bodi ya Cosad
 Baba Askofu Bagonza akisalimiana na Blogger Jamco, na kumpongeza kwa kazi kubwa a
 nayoifanya kuitangaza Bukoba na Kagera.
Blogger's wa Jamcobukoba.blogspot.com na Bukobawadau wakiteta kuhusiana na shughuri za Cosad.Endelea kufuatilia ufunguzi rasmi.

No comments:

Post a Comment