Sunday 8 June 2014

HALMASHAURI KUU YA WILAYA YA CCM MANISPAA YA BUKOBA WATOA TAMKO KUFUATIA OMBI LA FRIENDS OF BUKOBA KWA WAZIRI MKUU

 Katibu wa itikadi na uenezi wa wilaya ya Bukoba Mjini Ndugu Ramadhani Kambuga akisoma Tamko la Halmashauri kuu ya wilaya mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za chama Bukoba Manispaa,akiwa na Katibu wa Wilaya Bukoba Manispaa Janat Musa Kayanda na Katibu wa Uvccm Bukoba Manispaa
 Baadhi ya majina ya wana Friends of Bukoba wanaohishi nje ya nchi na ndani ya nchi
 Waandishi wa vyombo vya habari
 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Manispaa Bukoba Yusuf Ngaiza
 Ni baadhi ya kilichoandikwa katika barua iliyopelekwa kwa Waziri Mkuu
 Katika Barua hiyo hakuna mwanajumuiya yeyote aliesaini, wala kuonyesha sahihi ya kiongozi yeyote wa umoja huu kitu ambacho kimeleta mashaka .
 Hapa yanaonekana majina na anuani za barua pepee na hakuna mahala mwanajumuia yeyote aliposaini.
   TAMKO LA KAMATI YA SIASA YA HALMASHAURI KUU YA WILAYA JUU YA OMBI LA FRIENDS OF BUKOBA KWA WAZIRI MKUU  KUVUNJA MANISPAA YA BUKOBA.                                                                                                                                                   Kamati ya siasa ya wilaya katika kikao chake cha tarehe 06/6'2014 kilijadili kwa kina ombi la Friends of Bukoba kwa waziri mkuu kuhusu mgogoro wa Manispaa ya Bukoba.                                                       Kikao kilisikitishwa kuona wazawa wa mkoa wa Kagera waishio nje  na ndani ya Tanzania wakiomba Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kuvunjwa na Waziri Mkuu ili kufifisha maendeleo ya Wananchi ya Wananchi wa Bukoba huku wakijua wazi kuwa wanakiuka Demokrasia na kuvunja misingi ya utawala bora kwani chombo hiki kinaundwa na wananchi kidemokrasia. Wanajumuiya wa Friends of Bukoba wangekuwa wanawatetea wananchi waliotwaliwa ardhi zao na kubaki masikini wa kutupwa.Jamii na chama cha mapinduzi Bukoba mjini tungewaunga mkono.Aidha wangeibana Serikali kutekeleza ushauri wa taarifa ya CAG. Pia chama cha mapinduzi na wananchi wa Bukoba mjini tungeelewa kuwa Umoja huo una machungu na maendeleo ya wananchi. Huwa ni mvaaji anayejua wapi na kwa kiatu kinambana. Achilia mbali kwamba wenngi wa wanachama hawa wanaishi nje ya tena mbali na Manispaa ya Bukoba kimawazo,kiuchumi,kijamii na kimaendeleo lakini pia wameshindwa kuwa na mawazo shirikishi juu ya kuendelea ombi lao adui wa maendeleo ya wananchi wa manispaa ya Bukoba. Kiuhalisia inasikitisha sana kuona mtu au kundi la watu  likikimbia suluhisho hasi juu ya jambo wajivikalo kinadharia na mapenzi yao kuonekana tu mwishoni kwa waso la kuvunja na sio kujenga. Hii ni hatari katika Tsifa kama yatajikusanya makundi ya watu na kushinikiza serikali kufuta Halmashauri moja kwa njia ya maombi basi zitafutwa halmashauri nyingi nchini. Chama cha Mapinduzi Bukoba Mjini kimebaini kuwa Umoja huo lengo lake ni kutetea mtu au baadhi ya watu ambao hawapendi maendeleo ya wananchi  na wapo kwa maslahi yao binafsi. Chama cha mapinduzi Bukoba Mjini bado kinma imani mgogoro huu utakwisha na madiwani wataendelea kufanya kazi za wananchi na maelewano.Kubwa wapewe nguvu na uwezo  na serikari kuu kuchukua hatua za maamuzi. Kamati ya siasa na Halmashauri kuu ya Wilaya Bukoba Mjini inalaani na kupinga vikali ombi la Friends of Bukoba kwa waziri mkuu la kuvunja Hamashauri ya Bukoba.                                                                                               KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

No comments:

Post a Comment