Mwenyekiti
wa Bongo Movie, Bw Steve Nyerere akiongea na waandishi wa habari wakati
wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa East 24
uliopo Arcade house Mikocheni.
Steve
Nyerere akinadi kinywaji cha Windhoek ambao ndio wadhamini wakuu wa
sherehe ya Kutimiza Miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movies, Sherehe
itakayofanyika katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House Mikocheni
jijini Dar Es Salaam Ijumaa ya tarehe 28.
Rais
wa FM Academia Nyoshi Ali Sadat akiongea na wadau waliofika katika
ukumbi wa East 24 wakati wa utambulisho wa wasanii na bendi zitakazotoa
Burudani siku ya Sherehe ya Kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie
itakayofanyika katika ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House ijumaa ya
tarehe 28 Mwezi huu
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Mabibo Beer, Bw Jerome Rugemalila akiongea na
Waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa Bendi na wasanii watakaotoa
burudani ya nguvu siku ya sherehe ya Kuzaliwa kwa Bongo Movie
itakayofanyika tarehe 28 katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House
Mikocheni Jijini Dar.
Baadhi ya wasaniii wa Bongo Movies wakifuatilia kwa makini
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Benadetha Rugemalira (aliyeshika
kinywaji cha Climax) akifuatilia kwa makini matukio wakati wa
utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa burudani siku ya ijumaa
kwenye sherehe ya Kuazimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movie
Baadhi ya wadau waliohudhuria utambulisho huo uliofanyika katika ukumbi wa East 24
Mkurugenzi
Mkuu wa Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalira (kulia) akijadiliana
jambo na Meneja masoko wa Mabibo Beer, Jerome Rugemalira (pili kulia) na
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Bwa Steve Nyerere na Msanii wa
bongo movie Adam Kuambiana
Mwenyekiti
wa Bongo Movie, Steve Nyerere akijadiliana jambo na Katibu wa Bongo
Movie Mtitu wakati wa utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa
burudani wakati wa sherehe za kutimiza miaka mitatu ya kuzaliwa kwa
klabu ya Bongo Movie.
No comments:
Post a Comment