Wananchi Mkoani hapa
wameonekana kuwa na muamko zaidi wa Ulinzi Shirikishi baada ya kutoa taarifa
mbili zilizofanikisha kukamata misokoto 1,038 ya madawa ya kulevya aina ya bangi
pamoja na mirungi kilogramu 75.
Akizungumza na
Waandishi wa habari ofisi kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema kwamba katika matukio mawili
yaliyofanikisha ukamataji wa madawa hayo taarifa zake zilitolewa na raia wema.
Kaimu Kamanda Muroto
alisema kwamba, tukio la kwanza lilitokea tarehe 18.02.2014 muda wa saa 1:30
asubuhi maeneo ya Kituo Kikuu cha mabasi jijini hapa ambapo mtu mmoja aitwaye
Charles Ogaga Ayunga (38) raia wa Kenya na ni mkazi wa Taveta nchini humo,
alikamatwa na misokoto 1,038 ya Madawa ya kulevya aina ya bangi iliyokuwa ndani
ya boksi.
Akifafanua taarifa
hiyo Kaimu Kamanda huyo alisema kwamba, siku ya tukio mtuhumiwa alikuwa
anatokea maeneo ya Ngaramtoni akiwa kwenye Hiace na alipofika maeneo ya Kituo
Kikuu cha Mabasi alishuka akiwa na boksi na kutaka kupanda basi linaloelekea
Horiri wilayani Rombo lakini kabla hajapandisha boksi hilo kwenye basi hilo
watu walimshuku na kutoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi, ambapo askari
waliokuwa doria maeneo ya karibu walikwenda katika maeneo hayo na kufanikiwa kumkamata
mtuhumiwa huyo akiwa misokoto hiyo.
Mara baada ya
mahojiano mtuhumiwa alikiri kuumiliki madawa hayo ya kulevya aina ya bangi na
kueleza kwamba alikuwa anasafirisha kupeleka nchini Kenya.
Wakati
huo huo mtu mmoja aitwaye Philipo Santolin (25) Mkazi wa
Horiri wilayani Rombo alikamatwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi yenye
uzito wa kilogramu 75 ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye vifurushi tofauti
tofauti7.
Akifafanua tukio
hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP)
Gilles Muroto alisema tukio hilo la ukamataji lilitokea tarehe 19/02/2014 muda
wa saa 2:00 usiku maeneo ya Kaloleni jijini hapa.
Alisema siku ya
tukio wananchi walitoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi kwamba, kuna mtu
alikuwa anasafirisha madawa hayo katika gari aina ya Corolla lenye namba za
usajili T 162 AYW toka mkoani Kilimanjaro kuja Arusha, ndipo askari walipoweka
mtego maeneo ya Kwa Mrefu na mara baada ya gari hilo kusimamishwa halikusimama
ndipo askari wakaamua kulifuatilia ambapo walifanikiwa kulikamata maeneo ya
Kaloleni mara baada ya gari hilo la mtuhumiwa kupasuka tairi la mbele.
Kaimu Kamanda Muroto
alisema mpaka hivi sasa watuhumiwa wote wawili wanahojiwa na watafikishwa
makamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
No comments:
Post a Comment