Friday 28 March 2014

CAMERA YETU PANDE ZA HAMUGEMBE LEO DARAJA LA KANONI,NI MWEZI MMOJA NA SIKU CHACHE TANGU LIFUNGULIWE BAADA YA UKARABATI KUKAMILIKA NA KUTUMIA ZAIDI YA MILIONI 300 NA SASA LINAFANYIWA TENA

 Nakumbuka siku hiyo takribani mwezi moja na siku kadhaa zimepita maeneo ya daraja hili la Kanoni barabara kuu inayounganisha manispaa ya Bukoba na  Mikoa mingine ilikuwa ni furaha, nderemo na vifijo, huku wananchi chini ya Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Fabian Massawe wakishuhudia kwa macho na taarifa iliyojaa matumaini na weredi mkubwa kuhusu ukamilishaji wa ukarabati wa daraja hili la Kanoni. Kipindi hicho daraja hili lilipofungwa ilitokea adha kubwa kwa magari kupitia njia zingine ambazo zilisababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi ,lakini pia kwa madereva na kusababisha ajali na watu kupoteza maisha.Kwa taarifa iliyotolewa siku hiyo kwa mbwembwe na umaili mkubwa mbele ya mkuu wa mkoa kwa kutumia mamilioni ya fedha, leo ndani ya mwezi mmoja na siku  hali iko hivi.Hapa yapo maswali ya msingi sana kujiuliza ,Lakini kikubwa ni watu kutambua kuwa wale waliobahatika kupewa dhanana ya kusimamia masrahi ya watu watambue pia wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa wananchi, na zaidi ya hapo waende mbali zaidi kuwa Duniani  tunapita na kila kilichomo, ulichonacho , ulichokula, ulichokipata aidha kwa haki au vyoyote vile utaviacha na utahukumiwa kulingana na matendo yako.
 Ni  swala la kusubiri, maana hata pikipiki haiwezi kupishana na gari kutokana na ufinyo wa daraja kwa sasa
 Ni msongamano wa magari ambayo inabidi  yasubiri
 Hili ndio daraja ambalo upande mmoja  linafanyiwa ukarabati tena, na hali hii kusababisha msongamano

No comments:

Post a Comment