Wednesday, 26 March 2014

YALE MANENO YA KUFA KUFAANA YAMETIMIA UWANJA WA KAITABA BUKOBA KUFUATI UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA 2-5-2014

  Wa kale walinena  Kufa kufaana, maneno haya yametimia na kuleta faraja kwa wakazi wa manispaa ya Bukoba na Mkoa mzima wa Kagera kufuati ujio wa mbio za mwenge kitaifa zitakazozinduliwa rasmi 2-5-2014 katika uwanja wa Kaitaba.Yamekuwepo malalamiko ya muda mrefu sana kwa wapenzi wa soka kulalamikia ubovu wa majukwaa na miundo mbinu mbalimbali katika uwanja huu,Lakini kufuatia  tukio la uzinduzi wa mbio za mwenge yapo marekebisho makubwa yanaendelea katika uwanja huu, na Leo 26-3-2014 Mkuu wa Mkoa  wa Kagera Kanal Fabian Masawe alifika kujionea hali halizi ya maendeleo ya marekebisho ya uwanja nas kujionea  Wanafunzi  mia sita wa Halaiki wanaoendelea na mafunzo mbalimbali ya gwaride na nyimbo kwa ajili ya uzinduzi wa mbio za mwende Kitaifa Mkoani Kagera.
 Ni moja ya jukwaa ambalo linatengenezwa na litaezekwa juu kwa bati kumuwezesha mkaaji asipigwe na jua au kunyeshewa na mvua, na mbao zake zikiwa zimewekwa imara zaidi,
 Ukarabati ukiendelea
 Wanafunzi  mia sita wa shule za msingi katika baadhi ya shule Manispaa ya Bukoba wakiwa katika mafunzo ya Halaiki
 Kushoto ni Afisa Elimu shule za msingi Manispaa ya Bukoba Ndugu Fande akiwa na Afisa Utamaduni Manispaa Ndugu Rugeiyamu wakiratibu shughuli zote katika uwanja waKaitaba

 Ni Nesi akitoa huduma kwa wanafunzi wenye matatizo mbalimbali wanaoendelea na mafunzo ya Halaiki
 Muonekano wa Jukwaa

 Mkuu wa Mkoa Kagera Kanal Fabian Massawe akisalimiana na walimu wanaendelea kusimamia na kufundisha mafunza ya Halaiki wanafunzi
 Mwl J J Mugango(kulia) ni miongoni mwa walimu wanaofundisha na kushoto ni Ndugu Kilema Athuman Kambagwa mkufunzi wa Halaiki
 Mwl Alistidia ambae ni katibu  mkufunzi akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa
 Wanafunzi katika pozz tofauti
 Utapenda , vijana wanaweza
 Ni miongoni mwa alama ambazo wanafunzi wanafundishwa na wataonekana hivi
 Mwalimu anapokuwa kazini hakuna mchezo
 Ni manjonjo ya kila aina wanafunzi wa Halaiki haoo
 Hii ndio timu nzima

 Afisa utamaduni akimkaribisha Mkuu wa mkoa aongee na Walimu na wakufunzi

 Kanal  Fabian Massawe akiongea na wanafunzi kuwapa moyo na kuwataka pale kwenye mapungufu waongeze bidii

 Mkuu akikagua maeneo mengine
 Choo kipya kimejengwa katika uwanja wa kaitaba
 Hii ndio Kufa KUFAANA
 kAITABA inavyoo vya kufrash utapenda
 Jukwaa maarufu kama Jukwaa la Balimi nalo linaezekwa
 Jamcobukoba.blogspot.com tunatoa pongezi kwa uongozi wa kitaifa na mkoa kwa kuleta uzinduzi huu katika mkoa wetu,chini ya kapeti ziko habari kuwa uwanja huu hivi karibuni utawekewa nyasi bandia,yote ni heri kwa wana Kagera, ukizingatia Rais wa TFF NI...... Malizia mwenywe, Wahaya wanasema Eofisi etainamu wawe eikala ekomile. asante WAJINA.

No comments:

Post a Comment