Wadau sambamba na camera yetu wakiingia uwanja wa Taifa
Azam Tv wakiwa kazini
Mashabiki wa Yanga akishangilia
Ni mmoja wa mashabiki wa Yanga aliekuwa akifanya vituko uwanjani akiwa na njiwa wake
Wachezaji wa timu zote wakisalimiana kabla ya mpambano kuanza
Wachezaji wa Azam kabla ya mechi kuanza
Ni yanga walipopata gori
Yanga wakishangilia bao
Dakika
90 za Mtanange wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga na Azam Fc,
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, zimemalizika kwa Mabingwa
wa Soka Tanzania Yanga kulazimishwa sare na kufanya timu
Bao
la Yanga lilifungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 14 kipindi cha
kwanza huku bao la kusawazisha la Azam Fc, likifungwa na Kelvin Friday
katika dakika ya 83.
Katika dakika ya 70, Yanga walipata penati baada ya beki wa Azam, Said Morad, kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Penati
hiyo ilipigwa na Hamis Kiiza na kupanguliwa na kipa Aishi Manula, na
katika heka heka hizo Beki wa Azam Fc, Erasto Nyoni alizawadiwa kadi
nyekundu.
Kwa
matokeo hayo sasa Azam Fc inaendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo
ikiwa na jumla ya Pointi 44 huku Yanga ikibaki nafasi ya pili ikiwa na
pointi 40 lakini ikiwana na mchezo mmoja mkononi unaotarajiwa kupigwa
mwishoni mwa wiki mjini Tabora na Rhyno, na mbeya city wakibaki nafasi ya tatu.
Heka heka langoni mwa Azam Fc.
Heka heka langoni mwa Azam Fc.
No comments:
Post a Comment