Monday, 9 December 2013

SAFARI YA KINANA KUTOKA MAKAMBAKO- DAR ES SALAAM


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akipanda behewa na wasaidizi wake, Katibu wa NEC,
Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye (juu), wakati yeye na msafara wake waliposafiri kwa treni kwa zaidi ya saa 22, kutoka Stesheni ya Makambako na kuwasili Dar es Salaam, saa 12, 30,  Desemba 9, 2013,  kwa  teni ya
Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku 22, ya
kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua,
katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Treni ilitoka Makambako jana saa 2.30 asubuhi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akishuka kwenye behewa  na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (juu), kukagua stesheni ya Mlimba, mkoani Morogoro, wakati yeye na msafara wake waliposafiri kwa treni kwa zaidi ya saa 22, kutoka Stesheni ya Makambako na kuwasili Dar es Salaam, saa 12, 30,  Desemba 9, 2013,  kwa  teni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku 22, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Treni ilitoka Makambako jana saa 2.30 asubuhi.
 Dk. Asha-Rose Migiro na Nape wakishuka kwenye treni katika stesheni ya Mlimba, mkoani Morogoro
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa na Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Mlimba wilayani Kilombero mkoani Morogoro, Selemani Balali (kulia) aliposhuka na msafara wake, kwenye stesheni ya Mlimba, akiwa njiani kutoka Makambako kwenda Dar es Salaam, jana
 Kinana na msafara wake, wakiwa na viongozi wa Kata ya Mlimba, alipokwenda kukagua stesheni ya eneo hilo. Mbele ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
 Kinana, Dk. Asha-Rose Migiro na Nape Nnauye wakitoka kukagua jengo la stesheni ya Mlimba
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua karanga  kwa mwananchi aliyekuwa akifanya biashara ya karanga hizo kwemye stesheni ya Mlimba, Wilayani Kilombelo mkoani Morogoro
 Kinana akimlipa fedha muuzaji huyo wa karanga, Josephine  Amani
 Kinana akiuliza bei ya embe zilizkuwa zinauzwa na mwananchi kwenye stesheni ya Mlimba
 Kinana na Nape wakiuliza bei ya samaki kwa muuzaji wa bidhaa hiyo kwenye stesheni ya Mlimba, jana
 Dk. Asha-Rose Migiro na Nape wakitazama samaki waliokuwa wanauzwa kwenye stesheni ya Mlimba
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga stori na baadhi ya wasafiri kwenye stesheni ya Mlimba.
 Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na mmoja wa viongozi wa CCM waliompokea Kinana na msafara wake kwenye stesheni ya Mlimba
 Abiria akipitisha mtoto dirishani wakati treni inatoka Makambako
 Treni ikichana msitu kwenda Dar es Salaam
Treni ikipita katika 'tanuru' ndani ya mlima wakati ikitoka Makambako kwenda Dar es Salaam

MAPOKEZI DAR
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Madabida akimlaki Kinana kwenye stesheni ya TAZARA baada ya Kinana na msafara wake kuwasili Dar es Salaam leo asubuhi. Anayeshuka nyuma ni Dk. Asha-Rose Migiro.
 Kinana akiwa naNape, Dk. Asha-Rose na Madabida wakati akipita katika paredi la mapokezi la UVCCM, stesheni ya TAZARA
 Kinana na Nape wakiagana kwa furaha na waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wote, baada ya kuwasili stesheni ya TAZARA Dar es Salaam, leo asubuhi
 Kinana akimsalimia Kaimu Mkurugenzi wa UHURU FM, Angel Akilimali kwenye mapokezi hayo
 Kinana akisalimiana na Mbunge wa Temeke, Abbasi Mtemvu kwenye stesheni hiyo. Badaye Kinana alizungumza na wananchi waliofika kwenye mapokezi hao ambapo aliwashukuru sana kwa mapokezi huku akieleza kwamba WanaCCM aliokutana nao kwenyeziara yote wamemtia moyo wa kuendelea na ziara nyingine ya aina hiyo katika mikoa mingine.

No comments:

Post a Comment