Wednesday 11 December 2013

RAIS KIKWETE NA VIONGOZI WAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA NELSON MANDELA



unnamed_24e2b.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura Bush wakiwa jukwaa la viongozi na watu mashuhuri baada ya Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela leo Desemba 10, 2013 katika uwanja wa FNB jijini Johannesburg.
unnamed_1_ddc1a.jpg
unnamed_2_cdb96.jpg
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Desemba 10, 2013, ameungana na viongozi wa mataifa mbali mbali duniani na maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela.
Maelfu kwa maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa nguvu kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee Mandela ambaye alikuwa ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa rangi za makaburu wa Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment