Wednesday 11 December 2013

CAPE TOWN WAPITISHA BAJETI YA SH 12.2 BILIONI KUMUAGA MANDELA



mandela_8600e.jpg
Baraza la Jiji la Cape Town, limeidhinisha matumizi ya Rand72 milioni (Sh12.2 bilioni) kwa ajili ya mazishi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Taarifa ya baraza hilo iliyotolewa jana ilisema bajeti hiyo ilipitishwa katika kikao cha dharura na kwamba itasaidia kufanikisha shughuli zote za maandalizi ya kumuaga Mandela katika mji huo.
Mbali na kupitisha bajeti hiyo, pia liliamua kuweka usafiri wa bure kwa kutumia treni za mji huo – MyCiTi na mabasi marefu ya Golden Arrow kuwafikisha watu katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya kuonyeshwa shughuli za kuaga mwili.

No comments:

Post a Comment