Monday 9 December 2013

BUKOBA VETERAN WAHANI NYUMBANI KWA MAREHEMU HASSAN(HANS) MUNJURI NA KUBABIDHI RAMBIRAMBI ZAO,MWILI KUSAFIRISHWA 10-12-2013 KUPELEKWA KORONGWE TANGA

                                             Marehemu Hassan Munjuri katika uhai wake,Marehemu aliuwawa siku ya jumamosi majira ya saa tatu usiku maeneo ya bukoba coop hotel(yasila hotel zamani) kwa kupigwa risasi na mtuhumiwa ajulikanae kwa jina la Nasoro Robert ambae ni mhandisi wa wilaya ya Bukoba Vijijini  ambae ameshakatwa na police kwa uchunguzi zaidi.
 Mjane wa marehemu w kwanza kulia akipewa pole na ndugu, jamaa na marafiki waliofika kuhani
 Viongozi wa Bukoba veteran wakipanga jinsi ya kumuaga mwana veteran mwenzao
                                                    Kila mmoja anajiuliza kulikoni kilichotokea
                     Mmoja wa watoto wa marehemu, ameacha mjane na watoto wawili
                                                 Bw Mtensa akitafakari kifo cha Hans
 Bw Mkude akitangaza utaratibu wa kutoa  heshima za mwisho tarehe 10-12-2013 katika uwanja wa kaitaba kuanza saa 2.30 asubuhi na baada ya hapo mwili unapelekwa uwanja wa ndege na kusafirishwa kupelekwa Korongwe Tanga, Marehemu alikuwa ni mfanyakazi wa klampuni ya sigara Bukoba ambao wamekodi ndege ya kusafirisha mwili wake.
Pumzika kwa amani mpendwa wetu  Hans, tulikupenda sana ila mungu amekupenda zaidi

No comments:

Post a Comment