Saturday 16 May 2015

BALOZI KAGASHEKI ATIMIZA OMBI LA MWENYEKITI WA MTAA WA CHADEMA.

 Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Sued Kagasheki ametimiza ombi la mwenyekiti wa mtaa wa chadema kata ya kitendaguro Bwana Mweyunge Paulo Erasto,Katika nkutano wa hadhara wa Mbunge katika kata ya kitendagoro ,Bw Mweyunge alisimama akamuomba mbunge asaidie kuwapatia tochi,filimbi na betri kwa ajili ya kusaidia katika zoezi la ulinzi shirikishi katika kata hiyo kutokana matukio ya uharifu yaliyokuwa wamejitokeza kwa kasi kubwa katika kata ya Kitendaguro na Kibeta,Bw Mweyunge alimueleza mh Kagasheki kuwa pamoja na jeshi la polisi kujitahidi kupambana na waharifu, lakini pia wao katika mitaa saba ya kata Kitendaguro wananchi wameweka utaratibu wa kuzunguka usiku kucha kuhakikisha usalama wa wananchi unakuwepo.(Katika picha msaidizi wa Mbunge Bw Jumanne Bingwa akikabidhi vifaa kwa niaba ya Mbunge Kagasheki)
 Viongozi wa Kata Kitendaguro wakipokea vifaa.

 Mtendaji wa Kata ya Kitendaguro Bi Mary (gauni la njano) akipokea vifaa.
 Ofisi ya Kata .
Endelea kuangalia jamcobukoba.blogspot.com

1 comment:

  1. Safi Mh. Keep it up ila siyo kwa ajili ya uchaguzi 2015,maana mda kama huu ndo mnajifanya mna masiko makubwa kweli kusikia na kutekeleza maombi na ahadi ili tuawape kura mkare kifisadi!

    ReplyDelete