Monday 18 May 2015

ZOEZI LA UANDIKISHAJI DAFTARI LA KUPIGA KURA KUANZA RASMI 21-5-2015 KATIKA MANISPAA YA BUKOBA, VIONGOZI WAHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA

 Viongozi mbalimba wa kidini,serikari, vyama vya siasa na makundi mbalimbali wametoa wito na kuwaomba wananchi wanaoishi katika Manispaa ya Bukoba kujitokeza kwa wingi kwenye kata zao katika zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR linaloanza 21-5-2015 mpaka 20-6-2015,kwa mujibu wa maelekezo kutoka ofisi ya Manispaa Bukoba zoezi la uandikishaji litakuwa likifanyika kwa awamu katika kata,Kata za Rwamishenye,Kagondo,Nyanga,Ijuganyondo na Kibeta ndio zitakazoanza zoezi la uandikishaji kwa kipindi cha wiki moja na kuamia katika kata zingine,Kwa nyakati tofauti wakati wa mahojiano ya kipindi maalumu kilichoandaliwa na Bukoba cable Tv wakishirikiana na Jamco video production kitakachorushwa 
BUKOBA CABLE TV viongozi wamewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi.(katika picha ni Mchungaji  Elisha Bililiza msaidizi wa Askofu Angalikana.
 Katibu wa ccm Mkoa Kagera Bw Idi Ali  Ame amewataka wananchi wote katika Mkoa wa Kagera wajitokeze kwa wingi kujiandikisha.
 Bw Hamimu Mohamodu Katibu wa siasa na Uenezi Mkoa wa Kagera amesisitiza kila mtu ajiandikishe eneo analohishi ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza kwa udanganyifu wa eneo unalohishi.
 Baba Askof Methodius Kilain amewataka wananchi kutumia haki yao ya msingi kujiandikisha kwa wingi ili waweze kuchagua viongozi wanaofaa,Amesema kila mmoja anapaswa kutambua kuwa anaowajibu wa kujiandikisha maana ni haki yake ya msingi.
 Mbunge wa Bukoba Mjini Balozi Khamis Sued Kagasheki amewaomba wananchi wote wake kwa waume,vijana wote wajitokeze kwa wingi wajiandikishe,Pia amewataka watu wasiwe na shaka ,serikali na vyombo vya usalama wamejipanga vizuri kuhakikisha kila mwananchi wa eneo husika anajiandikisha bila kubugudhiwa.
 Bw Nelson , Mwendesha tax akitoa maoni yake.
 Bw Ramadhani Kambuga, nae akisisitiza jambo katika mahojiano.
 Katibu Mkuu wa KKKT Mch Elmereck Kigembe,amewakumbusha wananchi kuwa kuchagua viongozi ni wajibu wa kila mtu, sasa tumia fursa ya kujiandikisha ili badae uweze kutoa maamuzi.
Jamcobukoba.blogspot.com ikishirikiana na Bukoba cable Tv tunawashukuru wote waliotupa ushirikiano.

No comments:

Post a Comment