Tuesday 19 May 2015

SEMINA YA MAFUNZO YA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA YALIYOHUSISHA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR KITS OPERATOS YAFUNGULIWA LEO BUKOBA.

 Leo 19-5-2015 semina ya mafunzo ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura yaliohusisha waandishi wasaidizi na BVR KITS OPERATORS yamefunguliwa katika Manispaa ya Bukoba na mgeni rasmi alikuwa msaidizi wa katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Bw Seif Hussein, Katika hotuba ya ufunguzi mgeni rasmi  Bw Seif amewataka wanasemina wote kuzingatia mafunzo watakayoyapata ili kila mmoja aweze kutekeleza wajibu na majukumu yake katika kufanikisha zoezi muhimu sana la uandikishaji.(katika picha ni baadhi ya wanasemina)Mgeni rasmi Bw Seif Hussein
 Wanasemina.
 Bw Erick Bazompora ambae ni afisa uchaguzi akisisitiza jambo.
 Mashine zitakazotumika katika uandikishaji(BVR) ni kifaa cha kisasa ambacho huandikisha kwa kompyuta na kuchua alama za vidole,saini na upigaji picha kwa ubora wa hali ya juu ili kuondoa uwezekano wa wapiga kura kujiandikisha zaidi ya mara moja( na gharama ya mashine moja ni zaidi ya milioni kumi ya kitanzania).
  Bw George Herman Afisa (IT) akigawa vifaa kwa wanasemina.
 Kushoto ni  Bi Julieth John Afisa mwandikishaji  Jimbo, akiwa na  Bi Sarafina Rwegasira mwanasheria wa Manispaa.
 Bw Abdon Kahusa Afisa mwandikishaji msaidizi wa Jimbo.
A
 Afisa utumishi wa Manispaa akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo.
 Wanasemina wakijitambulisha.
 Wataalamu kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi.
 Wanasemina wakira kiapo.
Mwanasheria wa Manispaa akiwaapisha wanasemina.

No comments:

Post a Comment