Wednesday 13 May 2015

MANISPAA YA BUKOBA YAZINDUA MFUKO WA BIMA YA AFYA(CHF) MATIBABU KWA KUTUMIA KADI (TIKA)

Manispaa ya Bukoba imezindua rasmi mfuko wa jamii wa Bima ya Afya CHF  ambapo wananchi watapatiwa matibabu kwa kutumia kadi kwa kuchangia shilingi elfu kumi kwa mwaka,Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Jackson Msome kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella katika kikao kilichojumuisha wadau wa Afya na waratibu wa mfuko huo kutoka makao makuu.Bwana Msome amesema kuwa mfuko huo utawawezesha wakazi wa Manispaa kupatiwa matibabu kwa kutumia kadi (TIKA) kwa mwaka mzima na hivyo kuwaepusha na usumbufu wakati wa kutafuta pesa za matibabu,Mapema akisoma hotuba Mkurugenzi wa sera, Mipango ya Afya katika ofisi ya Katibu mkuu wizara ya afya, Mariam Ally amewataka wadau wa afya kuhamasisha wananchi katika Manispaa ya Bukoba kujiunga katika mfuko wa jamii wa Bima ya Afya kwa manufaa yao ya badae.
Washiriki wakijiandikisha kwenye ukumbi wa St Francis Bukoba.
Bwana Muchuruza(kushoto) Mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali KADETFU akiwa na Mzee Joansen Rutabingwa.
Mwanahabari wa CHF akiwa mambo sawa.
Mgeni rasmi akiwasili.
Washiriki .
Wafanyakazi wa Manispaa ya Bukoba.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Bukoba.
Mkurugenzi Mtendaji wa CHF akisoma rhotuba kwa washiriki.
Mkurugenzi wa sera, wizara ya afya Mariam Ally akitoa hotuba.
Wanahabari wakiwa kazini.
Naibu  Meya Alexandar Ngalinda akiwakaribisha washiriki.
Mgeni rasni Mkuu wa wilaya ya Bukoba Jackson Msome akitoa hotuba.
Diwani Robert Katunzi akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki.
Mkuu wa wilaya akipokea mashuka 150 yaliyotolewa na  CHF kwa ajili ya wagonjwa wa hospital ya rufaa ya Kagera.
muwezeshaji akiendelea na mada.
Wananchi changamkieni fursa.

No comments:

Post a Comment