Saturday 28 February 2015

KARAMAGI AENDELEA NA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA BUKOBA VIJIJINI,AZIDI KUWAMWAGIA VIFAA VYA MICHEZO VIJANA

Mnec wa Bukoba vijijini Mh Nazir Mustafa Karamagi ameendelea kwa kasi kubwa   kupita katika vijiji na kata za Jimbo la Bukoba vijijini kukutana na vijana kuzungumza nao na kugawa vifaa vya michezo na vizibao maalumu kwa ajiri ya waendesha pikipiki maarufu bodaboda.Akiongea na vijana katika nyakati tofauti maeneo ya Rukoma, Kibirizi,Kyaitoke, Izimbya na Mugajwale amewataka vijana wote washiriki katika michezo,na mtazamo wao usihishie tu kwa ajiri ya burudani, bali mtazamo wao uwe katika kutambua kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni ajira, na kuipitia michezo unaweza kujiajiri na kuendesha maisha,kwa upande wa bodaboda am,ewagawia vizibao maalum ili waweze kutambulika na nyakati za usiku  waweze kutambuliwa kirahi na waendesha magari barabarani kuepukana na ajari zisizo za lazima,Mh Mnec  anaendel;ea na ziara yake na anatarajia kuhitimisha ziara yake leo 28-2-2015 kwa kutembelea  kata 29 zenye vijiji 94 katika jimbo la Bukoba vijijini.
Vijana wakimsikiliza Mneck kwa makini.
Katika picha Mh Mnec akiwa na vijana ambao tayari wamekabidhiwa vifaa vya michezo.
Waendesha pikipiki wakiwa wameshakabidhiwa vizibao maalum.
Katibu wa wilaya Bukoba Vijijini ccm akiongea na vijana.
Mh Mnec akizungumza na wananchi.

Maneo mengi wananchi walijitokeza kwa wingi kumsikiliza Mnec na wengine walimpokea kwa nyimbo  na nderemo.
Waitu wakola ta Karamagi
Hii ndio hali halisi alikopita mh Karamangi, watu walifurika.
Tutaendelea kuwaletea matukio ya siku ya mwisho wa ziara yake, endelea kutembelea jamcobukoba.blogspot.com

No comments:

Post a Comment