Wednesday 25 February 2015

COSAD WAANDAA SEMINA YA KUWAFUNDA WASANII WA MUZIKI,WATAKIWA KUWA NA NIDHAMU WATAFANIKIWA.

 Mkurugenzi wa Cosad Tanzania Bw Smart Baitan akiongea na wasanii  wa muziki katika semina iiliyoandaliwa na Cosad, iliyofanyika katika viwanja vya eneo la studio za kurekodi za Cosad maeneo ya Kashura Kitendaguro Bukoba,Bw Smart amewataka wasanii kuwa na nidhamu na maadili ili waweze kufanikiwa,UKIBEBWA BEBEKA, NI maneno aliyoyatumia sana kwenye hotuba yake,Cosad ni shirika lisilo la kiserikali linalotoa huduma kwa jamii. Katika jitihada za kusaidia wasanii ,Cosad imefungua studio ya kisasa ya kurekodi kazi za wasanii wa muzii kwa gharama nafuu sana.
 Bw Smart akiwa na  Bw Izrael Kagaruki ambae ni Kipofu akieleza kwa kumtolea mfano kuwa  katika maisha usikate tamaa,Huyu Bw Izrael ni  kipofu  lakini ameshakuja marekani  mara mbili na akaendesha semina kubwa huko Marekani, kwa hiyo  kama wewe ni mkamilifu wa kila kitu kwa nini ulalamika na kushindwa maisha? Aliuliza bw Smart.
 Wafanyakazi wa Cosad.
 Mgeni rasmi akiwasili.
 Kwaya ya Tumaini ya Rwamishenye wakiimba moja ya nyimbo iliyorekodiwa katika studio za Cosad.
 Ma MC wakiendelea na utaratibu wa ratiba.
 Kushoto ni Mkurugenzi wa Kiroyera Tours Bi Ngonzi , mmoja wa wakufunzi waliotoa somo kwa wasanii.
 Msanii Teso boy akionyesha uwezo wake katika fani ya usanii wa filamu.
 Bw Teso boy muandaaji wa Mashindano ya NANI MKALI ambayo fainali zake zitafanyika siku ya pasaka na mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki.
 Mgeni rasmi akiongea na wasanii.
 Balozi Kagasheki akiongea na  Bi Victoria Kiwanuka ambae ni  Muuguzi mkuu katika dispensary ya Cosad iliyo Nyamkazi,alikuwa akifanya kazi huko Marekani na sasa amerudi kusaidia nyumbani.
 Bi Ngonzi Karikawe  Mkurugenzi wa Kiroyera Tours.
 Msanii Babu Rweyemamu akiteta na Mh Kagasheki.
Endelea kuangalia jamcobukoba.blogspot.com

No comments:

Post a Comment