Monday 16 February 2015

KAMANDA WA UVCCM MKOA WA KAGERA DIONIS MALINZI ASIMIKWA,NAPE ATEMA CHECHE.

 Katibu wa Itikadi , siasa na uenezi Taifa ccm Bw Nape Nnauye akimvisha joho kama ishara ya kumsimika kamanda wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw Dionis Malinzi katika uwanja wa uhuru plat form Bukoba.Katibu wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw  Didas Zihimbile akisoma taarifa .
 Bw Shafi akiweka mambo sawa.

 Ni Maandamano ya pikipiki na magari kueleke uwanja wa uhuru,baada ya mapokezi ya Nape.
 Bw Nape akiwa kwenye gari maalumu la wazi akiwa na Bw Dionis Malinzi.
 Saida Kaloli akifanya yake.


 Umati mkubwa ulioudhuria.
 Kushoto ni Bw Juliasi Rugemalila mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa ccm ,akiwa na mwenezi wa Bukoba mjini Ramadhani Kambuga.
 Kushoto ni Katibu wa ccm Mkoa wa Kagera  akiwa na Mbuge wa jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki.
 Mnec wa Bukoba Mjini Abdul Kagasheki akimtunza mtoto aliekuwa akicheza nyimbo za saida kwa ufasaha mkubwa ukilinganisha na umri wake.

Balozi Kagasheki akiongea na wananchi, kikubwa amesema,Nimechaguliwa na wananchi ili niwatetee, niwasemehe na kusimamia,katu hatomuonea aibu yeyote atakae taka kudhulumu haki za wananchi, akaongeza kuwa Siku zote unapowatetea wanyonge wapo watu wachache watakuzushia na kusambaza uongo, lakini yeye daima msimamo wake atabaki na wengi.
 Mwenyekiti wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw Yahya Kateme akiongea na wananchi, akizungumzia swala zima la uchaguzi , amesema vijana wako imara watasimamia na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi na ushindi utapatikana kwa kishindo.
 Mh Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella.
Siku zote wanawake uonyesha mapenzi ya kweli.

 Mh Dionis Malinzi akiwa ameshasimikwa,Bw Nape akiongea na wananchi wa amesema wananchi anawashukuru kwa kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi,na kwa hali ilivyo bado itaendelea kushika dora, amewataka viongozi  wa serikali Mkoa kuweka mambo yao sawa na hasa katika mgogoro wa Manispaa ya Bukoba, na amesisitiza kuwa wale wote waliohusika katika kuhujumu wananchi  hivi karibuni watapelekwa kwenye vyombo vya sheria,Pia akawashukuru wananchi wa Bukoba kwa kumuamini Mbunge wao Balozi Kagasheki na akasema ccm Taifa inatambua na kuthamini kazi kubwa anayoifanya Kagasheki na bado wanamuhitaji sana katika kulitumikia Taifa .





No comments:

Post a Comment