Saturday 12 April 2014

CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA KAGERA CHAFANYA MKUTANO MKUU WA KAWAIDA, JAMAL MALINZI ASEMA ATAENDELEA KUWA MWENYEKITI WA KRFA

 Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) kimefanya mkutano mkuu wa kawaida kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kagera na mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Missenye Kanal Issa Njiku. Awali akisoma taarifa yake mwenyekiti wa KRFA ambae pia ni Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi aliwashukuru wajumbe wote wa mkutano mkuu kwa namna walivyoshiriki kwa namna tofauti katika kuendeleza michezo katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera,Hotuba iliyosheheni mipango kedekede ya kuinua soka kwa ujumla  nchini Tanzania na Kagera ikiwemo.Katika mambo mengi aliyoeleza  ameweza kueleza changamoto nyingi zinazoikabiri KRFA na kuwataka viongozi kuhakikisha wanawasiliana na Halimashauri za wilaya zao kutenga maeneo ya viwanja vya michezo,akiongelea uwanja wa Kaitaba amesema anayofuraha kuwajulisha wajumbe kuwa sasa uwanja huo unawekewa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA kwa asilimia mia moja,lakini pia amehaidi kuitisha harambee ya wadau mbalimbali jijini Dar es salam kwa ajili ya kupata pesa ya kujenga jukwaa moja  katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.Pia aliweza kuelezea kuhusiana na nafasi ya uenyekiti wa KRFA, Amesema tangu amepata nafasi ya Rais TFF amekuwa akikutana na maswali mengi ya waandishi wa habari na wadau kuhusiana na kujiuzuru nafasi hiyo,( Wakati nakuja Bukoba nilikuwa na wazo ili la kujiuzuru ,lakini  kila mjumbe aliesimama hapa ameniomba nisijiuzuru mpaka wengine kutamka kuwa iwapo nitajiuzuru basi nao watajiuzuru nafasi hii,lakini kuna mjumbe kasema wapo watu wakati wa kampeni walikuwa wakisema natafuta nafasi hii ili niweze kugombea urais, kwahiyo basi naomba nitamke kuwa sitojiuzuru nitaendelea kuwa mwenyekiti wa KRFA.)
 Katibu wa KRFA Salumu  Chama akiongea na wajumbe
 Bw Pelegrius Rutayuga akisoma agenda za mkutano
 Mweka Hazina wa KRFA
 Mgeni rasmi Kanal Mstaaf Issa Njiku Mkuu wa Wilaya ya Missenye akifungua mkutano
 Wajumbe
 Bw Didas Zimbile mjumbe
 Bw Kazinja Mjumbe
 Mabrogger

 Makamu mwenyekiti wa KRFA
 Mkurugenzi wa sheria TFF Evodius Mtawala akifafanua vipengere mbalimbali katika marekebisho ya Katiba ya KRFA
Ukafika wakati wa


Katibu wa KRFA Salumu Chama akiwa na Mwenyekiti wa BUFA Marick Tibabimare

No comments:

Post a Comment