Hatimae uandikishaji wa wanafunzi katika chuo cha ualimu ERA kinachotarajia kuanza mwezi wa saba mwaka huu,Akiongea na mmiliki wa Blog hii ,Mwanzilishi wa chuo cha ERA kilichoko Bukoba Manispaa, kata ya Kitendaguro nje kidogo ya mji wa Bukoba Ndugu Paskazia Barongo amesema maandalizi yanaendelea vizuri na taratibu zote zinaendelea vizuri, ikiwa ni pamoja na kuandikisha wanafunzi wanaotarajia kuanza masomo mwezi wa saba mwaka huu.Amesema Ndugu Paskazia Barongo kuwa ni matarajio yao kuwa wamejipanga vizuri kutoa Elimu Bora ili waalimu watakaohitimu katika chuo cha ERA waweze kutoa elimu bora katika shule za msingi popote Tanzania kwa Weredi na ufasaha mkubwa,Pia ameeleza kuwa ile kuboresha mahusiano na vyuo vingine ndani na nje ya nchi chuo chao kimeanzisha urafiki na Global Citizens network walioko Minneapolis Marekani ili waweze kushirikiana katika maswala ya Elimu kwa wanafunzi wa ERA kwenda Marekani na wa Marekani kuja ERA. Ndugu Paskazia Barongo ameitaka jamii kwa ujumla kuleta watoto wao waliomaliza kidato cha nne na hawakuweza kupata nafasi wajiunge na chuo cha ERA na watajikomboa wao binafsi na kuwa Walimu wa mfano katika kutoa elimu bora nchini Tanzania.
Mama Ashura( Fundi cherehani) akimpima Unifomu mmoja wa wanafunzi anaetarajia kuanza masomo chuoni mwezi wa saba mwaka huu
Vipimo vya Unifomu
Bi Paskazia Barongo akiongea na wanafunzi wanaotarajia kujiunga na chuo, wakisubiri kupima Unifomu chuoni hapo
Bi Linda Stuart (kushoto) Mkurugenzi wa Global citizens network ya Marekani akiwa na Mkurugenzi wa Cosad Ndugu Smart Baitani anaeishi Marekani
Wanachuo watarajiwa wanaoanza masoma mwezi wa saba mwaka huu
bI Paskazia Barongo akiwakaribisha wageni
Mkuu wa Chuo cha ERA Bi Paulina Ngina Musau akieleza namna walivyojipanga kutoa Elimu katika chuo cha ERA
Mmoja ya wanachuo wanaojiunga akitoa neno la shukrani kwa kuanzisha chuo
Mwanachuo mtarajiwa akipongeza uongozi kwa wazo zuri la kuanzisha chuo cha ualimu
Mzazi akinukuu vifungu vya Biblia na kusema chuo cha ERA ni mkombozi kwa watoto wao
Wakipata kifungua kinywa
Mtoto wa Bi Linda Stuart akipata chai
Mkuu wa chuo akimtembeza kumuonyesha mazingira ya chuo na sehemu ya mabweni, katika chuo cha ERA Godoro na kitanda unavikuta chuoni ili kumpunguzia gharama mzazi
Ni vitanda imara na salama
Vyoo vizuri kwa afya ya wanachuo
Mazingira ya kupendeza
Bi Paskazia akitoa maelezo
Picha ya pamoja
Mkuu wa chuo Bi Paulina akiwa na mmoja wa wakurugenzi wa chuo ambae pia ni mwalimu katika chuo cha ERA Bw Ocham Collins wakiwa na mtoto wao
No comments:
Post a Comment