Thursday 10 April 2014

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA KAGERA AWASILI BUKOBA ,TAYARI KWA VIKAO VYA KIKATIBA

 Rais wa TFF ambae pia ni Mwenyekiti  wa chama cha soka Mkoa wa Kagera KRFA Jamal Emil Malinzi amewasili leo Bukoba katika uwanja wa ndege majira ya saa nne asubuhi na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa soka Mkoa, wadau na wapenzi. Atakapokuwa hapa mkoani atahudhulia kikao cha kamati tendaji ya KRFA kitakachofanyika leo na badae ataendesha na kusimamia mkutano mkuu wa kawaida wa KRFA, Lakini pia atapata fursa ya kukutana na viongozi wa serikali  ngazi ya Mkoa na Manispaa kuzungumza nao kuhusiana na maswala ya kimichezo.Rais wa TFF Jamal Malinzi akisaini kitabu cha wageni chumba cha mapokezi VIP Bukoba
 Akipokelewa na viongozi wa soka
 Mwandishi wa habari Audax Mtiganzi akiongea na  Bw Jamal Malinzi
 Rais wa TFF Jamal Malinzi akiwa na mshauri wa ufundi TFF bw Pelegrinius Rutayuga
 Al amin A bdul akimsalimia kwa bashasha Rais wa TFF
 Karibu sana mkuu,nitafurahi ukinikabidhi mikoba, ni maneno aliyoyatamka tukiwa hapo, sasa sijui ni mikoba ipi, mimi na wewe hatujui...

 Akaomba picha ya kumbukumbu
 Wakateta.....
 Akawasili Wily Kiroyera  wakasalimiana, angalia picha vizuri, kila mtu mawazo yakiwa tofauti
 Wily Kiroyera akisalimiana na Rais wa TFF
 akisalimiana na Katibu wa KRFA Salumu Chama
 Yakapita maneno ya utani......
 Mmiliki wa jamcobukoba.blogspot.com Jamal Kalumuna akiwa na Rais wa TFF, Hutaniana wajina
 Mdau Ruge Masabara,
 Mmiliki wa Bukobasports.blog Faustini Ruta akiwa na Rais TFF
 Msafara ulielekea Vctorius peach Hotel
 Didas Ziimbile akisalimiana na Rais wa TFF
 Al amin akiwa na Evodiua Mtawala alieambatana na Rais
 Hii ni picha itaingia kwenye Historia ya soka Kagera hivi karibuni




 Wadau mbalimbali wakiwa uwanja wa ndege Bukoba

Wapenzi wa soka wakiwa uwanja wa ndege

No comments:

Post a Comment