Monday, 3 March 2014

HAFRA FUPI YA UJIO WA MKOMBOZI COMMERCIAL BANK BUKOBA.

Mc wa Hafra hiyo Bw. Andrew Kagya akiwakaribisha wageni Ukumbini, Ukumbi wa Hoteli ya Coffee Tree iliyopo Bukoba Mjini, ambayo maandalizi yake yote yamegharimikiwa na kampuni yetu kupitia kinywaji maridadi cha Climax na Windhoek.
Taswira ya Vinywaji maridadi vya Climax na Windhoek.
Waimbaji wa Hapa Mjini Bukoba, Kapotive Star Singers-Bukoba walikuwa tayari kutumbuiza kwenye hafra hiyo ambayo lengo kuu la hafla hiyo ni kupata fursa ya kubadilishana mawazo wakati maswala ya kufungua tawi la benki la Mkombozi Commercial Bank hapa Bukoba.Bwana Respicius Didace wa Mabibo Beer wines & Spirits LTD akifunguka, Kwa niaba ya Kampuni yetu ya Mabibo Beer wine and Spirits, kupitia kinywaji chake cha kimataifa cha Windhoek Premium Lager 100% Pure African Beer na kinywaji kisicho na kilevi cha Climax Non Alcoholic Herbal Energy Welcome Drink, tunawakaribisha sana jioni ya leo kwenye hafla fupi ambayo ni muhimu sana kwetu wana Bukoba.

Leo tumebahatika kuwa na Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial bank ambae ataweza kutumegea machache kuhusu benki hii, na pia hata sisi tutapata nafasi kumuuliza maswali ambayo tunadhani yatasaidia katika kuongeza uelewa wetu kuhusu benki hii. Pia atatuonesha fursa zinazotokana na uwepo wa benki hii hapa Bukoba hasa kwa kununua hisa zake.

Kampuni yetu ya Mabibo Beer & Spirits Ltd inaamini katika kuwaleta watu pamoja, ndio maana wakati wa maandalizi ya hafla yetu hii, tumeawaalika wafanyabiashara wanaochipukia, wafanyabiashara wakubwa kwa kadiri ya mji wetu, viongozi wa dini, viongozi wa serikali, wawakilishi wa baadhi ya shule maarufu hapa Bukoba, wawakilishi wa wananchi kwenye kata (Madiwani) n.k. Hii ni fursa ya kufahamiana na watu mbalimbali katika nyanja mbalimbali wakati tunaendelea kuburudika na vinywaji vyetu vya Windhoek, na kwa wale ambao hawatumii kilevi wakifurahia Climax (Non Alcoholic Energy Drink).
Mr. Nicholas Mokirya-Branch Manager Mwanza Branch nae alikuwepo kwenye hafra hii na hapa alikuwa akitoa neno.Mheshimiwa mgeni rasmi, Mama Edwina Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank" akiwamegea machache kuhusu benki hiyo ya Mkombozi
Kulia ni Fr. Vitus Mrosso nae alikuwa tayari kwenye meza kusikiliza wito huo kwenye hafra hiyo swala zima likiwa ni kununua Hisa za Mkombozi commercial Bank ili kuweka akiba binafsi.
Wadau wakifuatilia kwa makini...
Bi. J. Murungi na Mr. Bube wakiteta jambo hapa wakati wa hafra hiyo
Mr. Bigambo (kushoto) nae alikuwepo mahala hapo
Lengo kuu la hafla hii ni kupata fursa ya kubadilishana mawazo wakati tunapoelekea kufungua tawi la benki la Mkombozi Commercial Bank hapa Bukoba.
Baadhi ya wafanyabiashara wa hapa Mjini Bukoba wakifuatilia kwa makini
Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba akisalimiana naWaziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Kapotive Star Singers-Bukoba wakiendelea kuimba nyimbo mbalimbali
Kapotive Star Singers-Bukoba wakicheza Ngoma  wakati wa hafra hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe akiteta jambo.
Taswira Ukumbini hapo Coffee Tree Hotel katika hafra hiyo iliyokuwa chini ya ya Uzamini wa Udhamini wa Windhoek and Climax.
Fr. Vitus Mrosso akiuliza swali kuhusu swala zima la Benki hiyo ya Mkombozi na Mikopo yake
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe (kulia) wakifurahia jambo kwenye meza kuu wakati wa hafra hiyo.
Meza kuu
Bi. Jeniffer Murungi Kichwabuta nae akiuliza swali kuhusu Hisa za Benki hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe(katikati) akijibu maswali
Bi. Edwina Lupembe hakuishia hapo kujibu maswali tu aliendelea pia kuwapa faida za benki hiyo ya Mkombozi na kuwataka wakazi wa Bukoba kuendelea kununua Hisa kwa wingi zaidi.
Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba (kulia) akitoa neno, Benki ya Mkombozi ni sauti ya kinabii inayolenga kuwaletea watanzania ukombozi wa kweli. Benki ya Mkombozi iliyozinduliwa mwaka 2009, kwa kianzio cha mtaji wa Shilingi Bilioni sita nukta nane, mchango wa waamini wa Kanisa Katoliki, inalenga kuwasaidia watu wa kipato cha chini kuinua hali yao ya maisha na wawekezaji kupanua kiwango chao cha kuwekeza kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote pasipo na ubaguzi.Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba (kulia) akionesha juu kwa wale ambao hawatumii kilevi wakitumie Climax (Non Alcoholic Energy Drink). Ambapo maandalizi yote yamegharimikiwa na kampuni kupitia kinywaji maridadi cha Climax na Windhoek.
Hata na mimi natumia kinywaji hiki cha Climax  (Non Alcoholic Energy Drink) Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba akikinanga kinywaji hicho!
Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki Bukoba, ni kati ya wajumbe wa Kikosi kazi, waliopewa dhamana kushughulikia mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Mkombozi nchini Tanzania. Hii ni sauti ya kinabii, katika mapambano dhidi ya umaskini. Ninakualika sasa uweze kujiunga na Askofu Msaidizi Kilaini kwa ufafanuzi zaidi kuhusu dhamana ya Kanisa ndani ya Jamii na Benki ya Mkombozi.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka nae aliguswa na Kinywaji hicho cha Climax
Rahim Abdul Rahim Kabyemela akipongezwa na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka  kwa kazi nzuri anayoifanya hapa Bukoba akiwa yeye ndie Balozi na msambazaji wa Vivywaji hivyo vinavyopendwa hapa Kagera.

No comments:

Post a Comment