Monday 3 March 2014

AFYA YA MWANDISHI WA HABARI WA STAR TV NA RFA YAZIDI KUBOREKA,WADAU WAMTEMBELEA NYUMBANI KWAKE KARAMBI NGOTE MULEBA

 Hali ya afya ya mwandishi wa habari wa Star TV na RFA  Raymond Owaman  inaendelea vizuri,  pichani kama unavyomuona akionyesha maendeleo ya afya yake,kwa muda mrefu sasa alipatwa na ugonjwa wa kiharusi uliosababisha baadhi ya viungo vya mwili kupooza na kushindwa kutembea na kukosa nguvu kabisa,kwa sasa hali yake inazidi kuboreka na kuonekana mwenye furaha na kuweza kuongea na kutamka vizuri, kitu ambacho mwanzoni hsakuweza hata kuongea na kutambua,
 Wadau wakiwasili nyumbani kwa Bw Raymond Owaman
 Mmiliki wa jamcobukoba.blogspot.com  Jamal Kalumuna (Jamco) akisalimiana na Mwandishi Raymond Owaman nyumbani kwake  Karambi Ngote Muleba
 Bw Raymond alijisikia faraja sana na furaha yake akaionyesha wazi,maana hakutegemea kama anaweza kupata wageni ghafla bila taarifa.
 Mke wa Bw Raymond Owaman
 Wadau waliofika kumjulia hali
 Akielezea hali ya maisha yake tangu ameugua na hali halisi ya maisha ya kijijini
 Hii ni picha ya ajari ya ndege iliyotokea 1-5-1997, ni moja ya matukio aliyoripoti kwenye vyombo vya habari, akiwa katika hekaheza za kazi zake
 Picha ya pamoja
 Picha ya pamoja wadau waliokwenda kumtembelea Bw Raymond Owaman
jamcobukoba.blogspot.com inawaomba wadau mbalimbali wafike kumtembelea na kumjulia hali Bw Raymond Owaman, kumfariji na kumpa moyo

No comments:

Post a Comment