Picha ya Balozi Wilson Masilingi iliyobandikwa nyumbani kwa mwananchi Karambi kata ya Kimwani Jimbo la Muleba Kusini
Mzee George Bwahama( Diwani mstaafu na mwenyekiti wa mtaa) ambae ameeleza kilio cha wananchi wa Karambi kuhusiana na kero za wananchi kutokuwa na ufumbuzi,amesema matatizo yanayowakabiri wananchi yamekosa majibu na ufumbuzi kwa kushindwa kuonana na mwakilishi wao waliomchagua na kusababisha kukata tamaa na kupelekea wananchi wengi kumkumbua alie wahi kuwa mbunge wao Wilsoni Masilingi ambae kwa sasa ni Balozi, Bw George amesema katika kipindi cha uongozi wa Masilingi alikuwa akipata muda wa kukaa na wanachi na kuskiliza kero zao na kuzitaftia ufumbuzi,kitu ambacho kwa sasa ni kama ndoto nma wao kuonekana kama wametengwa, amesema ipo migogoro ya ardhi,matatizo ya huduma za afya, miundombinu, maswala ya elimu nk, yote haya ni kero kwa wananchi ya karambi, akiongelea swala la elimu, amesema katika kipindi cha Masilingi aliweza kuwajengea shule ya sekondari kwa kuchangia kwa asilimia kubwa kutafuta wafadhili na nguvu za wananchi, na akasema shule hiyo ndio mkombozi kwa wananchi wa Karambi.
Eneo la kijiji cha Karambi
Tatizo la maji katika kijiji cha Karambi
Mazingira ya shule ya Sekondari Karambi ambayo ujenzi wake ni nguvu ya Balozi Masilingi
Majengo ya Sekondari ya Karambi ,jitihada za Balozi Wilson Masilingi kufanikisha ujenzi
Mazingira ya shule
Moja ya eneo korofi Karambi
Wananchi wa Karambi wakiburudika
Wananchi baadhi wa Karambi, walioelezea mgogolo wa ardhi uliopo eneo la Burigi lililovamiwa na wahamiaji haramu,walieleza kilikaa kikao kati ya wananchi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Prof Anna Tibaijuka tarehe 4-4-2013 mpaka sasa ufumbuzu haujapatikana,japo Waziri alihaidi kutatua mgogolo huu hakuwahi kurudi tena,huwa tunasikia amekuja anahishia muleba kwake huku haji( NI MAELEZO YA MMOJA WA WANANCHI)
No comments:
Post a Comment