Kagasheki cup 2013 inayoelekea hatua ya robo fainali itafungwa kwa muda kuanzia 22-7-2013 ili kupisha mkutano wa hadhara wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Jakaya mrisho kikwete utakaofanyika katika uwanja wa kaitaba 24-7-2013, kwa mujibu wa maelezo ya mwenyekiti wa kagasheki cup marick tibabimale amesema amea pokea barua kutokakwa mkurugenzi wa manispaa ikimtaka asitishe mashindano mpaka baada ya mkutano wa rais kikwete kufanyika.
wakati huohuo leo timu ya bakoba imeendeleza wimbi la ushindi la kuifunga kahororo 2-0 mechi iliyochezwa mapema na mechi ya pili hamugembe kamfunga nyanga 3-0
balozi kagasheki ambae ndio mdhamini wa mashindano haya ambayo yanazidi kupamba moto na kukusanya maelfu ya wanachi wanaojitokeza kutizama michezo mbalimbali katika uwanja wa kaitaba
uwanja huu ndio utakaotumika kwa ajiri ya mkutano wa rais kikwete 24-7-2013, hivyo mechi za tarehe 22-7-2013- 24-7-2013 zitapangiwa tarehe nyingine
kamati inaomba radhi kwa wapenzi wote wa soka, timu zote zitakazositisha michezo katika tarehe hizo,kwani swala hili ni la kitaifa.
No comments:
Post a Comment