KIGOGO WA DAWA ZA KULEVYA ATIWA MBARONI
Vita
dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya ni ya dunia nzima ambapo
kila nchi inafanya kila liwezekanalo kutafuta vyanzo vya mitandao
mikubwa inayofanya biashara hiyo. Serikali ya Mexico imefanikiwa
kumkamata kiongozi wa mtandao mkubwa wa matukio ya kihalifu na
usambazaji wa dawa za kulevya nchini humo unaofahamika kama ‘Zest’
aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba Taarifa iliyoripotiwa na
Reuters inasema mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina la Miguel Angel
Trevino aka Z-40, alifanikiwa kukamatwa jana (July 15) baada ya askari
kuifuatilia gari yake ya Pickup kwa helicopter.
Msemaji wa serikali
ya Mexico Eduardo Sanchez amesema, Trevino ( 40), alikamatwa akiwa na
washirika wake wengine wawili kufuatia operesheni ya miezi mingi ya
kumsaka, na alikutwa akiwa na pesa taslim zaidi ya $2 million.
Kukamatwa
kwa Z-40 ni ushindi mkubwa kwa serikali ya Mexico kutokana na ukubwa wa
mtandao huo wa Zetas ambao umekua tishio nchini humo kutokana na
vitendo vya matukio ya mauaji yaliyofanywa na magenge ya mtandao huo
unaojihusisha pia na biashara haramu ya dawa za kulevya, vitendo ambavyo
vimechafua jina la nchi hiyo kiasi cha kuwapa hofu watalii na
wawekezaji
No comments:
Post a Comment