Sunday 1 November 2015

BUKOBA WAMPONGEZA MAGUFULI KWA USHINDI,KAGASHEKI AWASHUKURU WANANCHI NA KUTOA UFAFANUZI KUHUSU UPOTOSHWAJI KATIKA MITANDAO.

 Maelfu ya wapenzi wa ccm Bukoba mjini walijitokeza kwa wingi katika makao makuu ya ccm mkoa wa Kagera na kutembea kwa mguu mpaka katika uwanja wa uhuru plat form kusherekea ushindi wa Dk Pombe Magufuli kushinda nafasi ya urais,Maandamano hayo yaliongozwa na aliekuwa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki,Balozi Kagasheki alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wote waliompa kura na kumpongeza Bw Wirfred Rwakatare kwa ushindi,pia akatumia nafasi hiyo kueleza na kuwataka wananchi kupuuza uzushi unaoenezwa kwenye mitandao kuwa baada ya kushindwa amechukua vitu alivyokuwa amevitoa kwa wananchi, Balozi kagasheki amesema kuwa kuhusu gari la kubeba wagonjwa Ambulence aliyonunua mwenyewe ilikuwa imeandikwa maandishi OFISI YA MBUNGE JIMBO LA BUKOBA MJINI NA NAMBA ZA SIMU ,Kilichofanyika ni swala la kisheria kufuta maandishi kwa sababu yeye si mbunge tena, hivyo litaendelea kutoa huduma kama kawaida kwa wananchi likiwa palepale lilipokuwa linatolea huduma katika ofisi yake,Kuhusu Tv kubwa aliyonunua kwa ajili ya watu kuangalia nyakati za jioni katika uwanja wa uhuru alisema amekuwa akilipa umeme na gharama zote za kuhudumia wananchi, kwa kuwa si mbunge tena alimtuma mtu awasiliane na uongozi wa Manispaa ya Bukoba kujua ni utaratibu upi utatumika kulipia gharama za tv hiyo kutoa huduma, kilichomshangaza na kumstua ni pale afisa utamaduni wa Manispaa ya Bukoba aliposema kuwa hiyo tv ililetwa na Regnard Mengi, kauli hiyo ilimstua sana na kushangaa kuona Bw Rugeiyamu anatoa majibu ya namna hiyo, Balozi Kagasheki amesema wananchi wapuuze habari hizo,amesema mbona awazungumzii mashule aliyojenga kwa pesa zake mwenyewe ,shule ya sekondari Buhembe,sule ya sekondari Bilele, shule ya sekondari Rwamishenye, kashabo, kitendaguro nk,Balozi kagasheki akasema kipindi chote cha kampeni walipanda majukwa wapinzani wakisema hakuna alichokifanya, sasa ambulence tu kufuta maandishi wameongea, mwanzoni mbona hawakutaja?Amewataka wananchi kupuuza, uchaguzi umekwisha na maisha yanaendelea,kikubwa amani na utulivu vitawale watu waendelee na maisha maana kikubwa ni kushika dora na Magufuli ndio rais wa Tanzania na si vinginevyo, sera itakayotekelezwa na vyama vyote ni sera ya ccm.
 waendesha pikipiki wakijiandaa kushiriki maandamano ya kumpongeza Magufuli.

No comments:

Post a Comment