Monday 2 March 2015

KARAMAGI AHITIMISHA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA KWA KUWEZESHA VIFAA VYA 65 MILIONI,VIJANA WAMKUBALI BUKOBA VIJIJINI.

 Hatimae Mnec wa Bukoba vijijini Mh Nazir Karamagi amehitimisha ziara yake ya kuimarisha chama katika jimbo la Bukoba vijijini kwa kutembelea kata 29 zenye vijiji  94 kwa kuongea na vijana na wanachama kwa kutoa vifaa vya michezo na vikoti maalumu kwa bodaboda .Mh Karamagi akiongea na blogger wa mtandao huu katika kipindi maalum amesema amefarijika sana kwa kazi kubwa iliyofanyika katika jimbo la Bukoba vijijini kwa kutana na vijana na kuongea nao na kusikiliza kero zao,lakini pia kupata wasaa wa kuwagawia vifaa vya michezo kwa ajiri ya kukuza viwango vyao na kupata vitu muhimu kama jezi, mipira katika mchezo wa soka,lakini pia amekutana na waendesha pikipiki  ambao amewagawia vikoti maalum vyenye thamani ya milioni 25 na vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 40 na kufanya jumla ya yote kuwa milioni 65. Mh Karamagi ambae kipindi cha nyuma aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Bukoba vijijini  amesema moja ya kazi kubwa  ya Mnec ni kuimarisha chama na kuwezesha kutatua changamoto mbalimbali zinazowasumbua wananchi,Mh Karamagi amesema mbali na ziara hii ya kuimarisha kata pia katika jitihada za kumuunga mkono Rais Kikwete katika ujenzi wa maabara amechangia mifuko hamisini ya saruji kwa shule zote za sekondari katika jimbo la Bukoba vijijini, lakini pia amewawezesha vikundi mbalimbali vya akina mama waweze kupambana na umasikini,Mh Karamagi amesema kwa hiyo hili alilofanya ni muendelezo wa mengi ambayo ameshafanya katika jimbo la Bukoba vijijini., na ataendelea kuimarisha chama.
 Katibu wa ccm Mkoa wa kagera akiongea na wananchi katika kata ya Kemondo wakati wa hitimisho  la ziara ya Mnec Karamagi.

 Mnec akikabidhi vifaa vya michezo.
 Waaendesha pikipiki wakiwa katika vazi maalum.
 Diwani viti maalum Amida Adam akiongea na wanachi.
 Mwenyekiti wa vijana Mkoa wa Kagera Yahya Kateme akimpongeza Mnec kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa vijana.
 Katibu wa Vijana Mkoa wa Kagera Didas Zimbihile.
 Mikutano ya mnec.
 Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Mkoa wa Kagera Revina Jovin akimwaga sera.
 Bi Geogia George msaidizi wa Mnec katika shughuli zake.
Endelea kuangalia jamcobukoba.blogspot.com

1 comment:

  1. Hivi NDITA zilizokunjwa na Vijana,zinaashiria TAFAKURI,HASIRA,au Ndo tunaimba kibepari na kucheza kijamaa!

    ReplyDelete