Thursday 16 October 2014

KITCHEN PART YA MAINDA KASSIMU NI NOMA,BWANA HARUSI MTARAJIWA ATINGA UKUMBINI KWA DAKIKA KADHAA NA KUONDOKA.

 Mwanahawa Kassim(maarufu kwa jina la Mainda)akitabasamu na mwenye bashasha kubwa akiwa katika ukumbi wa Lina's ikiwa ni siku kubwa sana kwake,Wamama kutoka maeneo ya kila kona ya mji wa Bukoba na maeneo mbalimbali walijitokeza kwa wingi sana kuja kwenye shughuri yake ya Mjuburo kumuaga.
 Mama Rukia,au Mama mzazi wa Mainda akiwa katika bango maalumu la kupigia picha lililoandaliwa ukumbini.
 Ni Wamama waliopendeza na nguo zao zenye rangi zilizosheheni ukumbi mzima,wamama walipendeza sana.
 Bi Shukuru akicheza akiwa amekaa,nao ni utaalam wanaweza wachache.
 Kushoto Mama Rukia akiwa na Mama Musa.
 Wadada wadogo kwa umbo na umri ,lakini wakubwa kwa mahiri kwa kuzungusha viuno,ilikuwa ni hatariiii.
 Mainda akijimwayamwaya kwenye bango la picha.
 Anakuja eheee kapendezaaaaa, duh.
 Mainda akiingia ukumbini akicheza kwa raha zake.
 Keki ya aina yake.
 Ukumbi ulifurika,si kitu cha kawaida.
 Hutaki unaacha,mmm Pinda Mugongoooo.
 Christa akicheka na camera yetu.
 Kulia ni Mama Mtaalamu wa keki.
 Mama nakupenda karibu keki.
 Mwanangu nakupenda karibu keki.
 Dada Rukia nakupenda karibu keki kazi yako nimeiona ,nilikuwa mbali umeangaika sana kuandaa nakushukuru sana dada yangu mpenzi.
 Wifi nawe njoo upate keki.
 Ikafika wakati Mainda akafanya bonge la suprise, akatoka ukumbini na aliporejea akaja na kitu pembeni.
 Mmmm ingekuwa video usipime wamama walizungusha viuno usipime.
 Ghafla watu wakazuka eneo la tukio.
 Nini tena hii nayo kali amekuja ukumbini,hawa wa mama wanajiuliza.
 Karibu mme wangu mtarajiwa ni kakutambulishe kwa wamama,wakujue na kuanzia leo watambue kabisa tayari umesajiriwa na namba yako ni Mainda.
 Mkwe mkubwa katika familia Bw Simba na mkewe Rukia(kushoto) akiwa na Bw Jamal Rashid na mkewe Mainda.
 Mainda mbele ya umati mkubwa wa wamama akachukua kipaza sauti ili kila aliepo na asie kuwepo ujumbe umfikie akasema wamama nawashukuruni kwa kufika huyu nilienae hapa ndio raazizi wangu Jamal Mwana wa Rashidi.
 Rashid nae akasema kwakuwa umetamka hadharani mchana kweupe nami nakuvisha pete ya uchumba.
 Mama akatoa zawadi kwa mkwe mkubwa.
 Mama akatoa zawadi kwa mkwe mdogo.
 Mama akatoa zawadi kwa mwanae.
Mainda nae akatoa zawadi kwa mama,chozi la furaha likamdondoka.
 Machozi ya furaha yakawatoka.
 Wamama wa mjini utawajua tu.
 Wadada wa mjini.
 Wamama na wadada wa mjini.
 Maisara na mdogo wake walishindwa kujizuia.
 Wanasema kumwaga radhi.
 Mainda akiwa na wifi yake,Dada wa mme wake mtarajiwa.
Jamcobukoba.blogspot.com inawatakia maandalizi mema ya ndoa 17-10-2014 na sherehe ya kuwapongeza itakayofanyika 18-102014 katika ukumbi wa Lina's.

No comments:

Post a Comment