Tuesday 3 June 2014

CAMERA YETU LEO KASHOZI ROAD BUKOBA AJARI

 Ni  majira ya saa nne asubuhi barabara ya kashozi karibu na  barabara inayoingia Banana Hotel gari kubwa  la kampuni ya Mecco inayokarabati uwanja wa ndege wa Bukoba lilimgonga mwendesha pikipiki na dereva wa gari hilo mwanamke hakuweza kusimama na kukimbia, na pikipiki kuharibika na kupelekwa polisi baada ya askari wa usalama barabarani kufika katika eneo la ajari. Jitihada za kumpata dereva huyo mwanamke pekee katika kampuni hiyo zinafanywa. Zimekuwepo ajari nyingi katika barabara hii ya kashozi kutokana na ufinyo wa barabara na watumiaji watembea kwa miguu na magari kuwa wengi zaidi , na hasa wakazi wanaoishi Kashai kutokana na barabara ya zamani kufungwa kutokana na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Askari wa usalama barabarani wakipima eneo la ajari
 Hapa ndio ajari ilipotokea  kati ya Gari la kampuni ya Mecco na pikipiki
 Umati wa watu wakiwa katika tukio

 Kushoto ni mtangazaji wa Kasibante redio akiongea na wananchi walioshuhudia tukio la ajari
 Barabara hii ya Kashozi inakuwa na msongamano mkubwa nyakati za asubuhi na nyakati za jioni hali inayochangia kwa kiasi kikubwa ajari kutokea kutokana na ufinyo wa barabara. Ni wakati muafaka sasa serikali kuliona hili mapema vinginevyo  huko mbele linaweza kutokea tatizo kubwa zaidi
 Ramani ya ajari ikichorwa
 Pamoja na jitihada za Askari wa usalama barabara, bila kupatikana ufumbuzi wa barabara mbadala itakuwa shida
 ENEO LA AJARI
 Ramani ya ajari
Barabara mbadara inahitajika haraka kunusuru maisha ya wananchi.

No comments:

Post a Comment