Misaada toka kwa Bi Gladness Sariah wa Uingereza, Dar es salaam kwa Norah SilverBoutique |
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwakilisha msaada toka kwa familia ya mama Masawe wa DSM kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha NURU kilichopo Uyole, mkoani Mbeya. |
-----------------------
Kituo cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya Yetu (www.mbeyayetu.blogspot. com) kimepokea
Misaada mbalimbali kutoka kwa wasamaria wema kwa ajili ya Kituo cha
kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya na Aida
Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa
Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa
kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini
Mbeya.
Kituo cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya Yetu (www.mbeyayetu.blogspot.
Msaada
wa kwanza ulipokelewa hivi karibuni wenye thamani ya shilingi Laki Moja
kutoka Familia ya Masawe wa Dar es salaam kwa ajili ya kituo cha Nuru
ambapo Mbeya yetu iliuwasilisha kama ulivyo.
Mbali na msaada huo pia Mtandao huu ukishirikiana na mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam wa www.issamichuzi.blogspot.com ulipokea
kutoka kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye
alitoa maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.
Aidha
katika kuonesha wengi wameguswa na tukio la Mwanamke huyo kujifungua
watoto wanne ambao wanaendelea vizuri, pia Msamaria mwema mwingine
aliyejulikana kwa jina la Dada Norah SilverBoutique toka Dar es salaam naye ametoa Maziwa Lactogen makopo 24 pamoja na nguo ambavyo vimewasili salama katika ofisi ya Mbeya Yetu.
Shukrani
kwa Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na
ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hii
Mbeya.
Kutokana
na kupokelewa kwa mizigo hiyo ambapo kituo cha Nuru kilikabidhiwa
Katoni Mbili za Sukari, Sabuni na Biskuti pia Tunatarajia kuanza safari
ya kwenda huko Chiwanda Wilaya ya Momba Kilomita zaidi ya 260 toka
Mbeya mjini kufikisha misaada ya Mama wa mapacha wanne.
Hivyo
ni wito wetu kwenu kuendelea kutuombea na kutuunga mkono katika safari
hiyo ili tuweze kuifikisha salama mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na
kuangalia maendeleo ya Watoto hao ambapo watakuwa wameshatimiza mwezi
mmoja na siku 24.
Tunawashukuru sana tena sana wote mliojitolea na Mungu awabariki sana.
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com
Nasi tutafikisha ubani wako.
Wazee wa Kazi Serengeti Freight wametoa ofa ya
kusafirisha bure misaada ya aina hii toka Uingereza.
Mbarikiwe sana Wazee wa Kazi.
No comments:
Post a Comment