Monday 24 February 2014

MASOGANGE NA MISS TANZANIA WALIVYOWAPAGAWISHA WAKAZI WA DODOMA KWENYE CAR WASH GIRL'S PARTY DODOMA


 Miss akiosha kati ya magari yaliyofika kupata huduma ya kuoshwa wakati wa 'CAR WASH GIRLS PARTY DODOMA' iliyofanyika jana mjini Dodoma, ambapo baadhi ya washiriki wa pati hiyo walikuwa ni Masogange, na baadhi ya mamis Tanzania wa mwaka jana.

 Masogange na Mrembo wakisebeneka jukwaani kuonyesha umahiri wao wa kunyonga kiuno, na kuwapagawisha watu waliokuwapo katika pati hiyo walioamua kuinuka vitini na kuwatunza mahela, wakati wa 'Car wash girls party'. 
Warembo waliokuwa vitini walishindwa kuvumilia na kuamua kuinuka na kwenda kutunza kama hivi. 

 Chezesha Kiuno, Chezesha kiunooooooooo......
 Tweeende saaaaaaaasaaaa.....
 Ale nyonga, nyongaaaa, nyongaaa.........
 Pembeni ni wadau wakiendelea kula Bata na Biere kwa raha zao huku wakipata burudani kutoka kwa kina Masogange.....
Hata wapendanao pia walifika kushuhudia kitu hiyo.....

No comments:

Post a Comment