Saturday 11 May 2013

HEKARU LA PROFESA ANNA TIBAIJUKA LILOJENGWA KATIKA SHAMBA LA MIGOMBA MULEBA

            Si jina geni masikioni mwako ukisikia jina la profesa Anna Tibaijuka,kila mmoja ananamna anavyomtambua,kwa ufupi ni mama makini mchapakazi anapokuwa kazini,Profesa anna ni mbunge wa muleba kusini,lakini pia ni miongoni mwa wabunge wachache waliobahatika kupata uwaziri katika serikari ya awamu ya nne ya rais jakaya kikwete,                            Nikiwa katika mizunguko yangu ya kutafuta riziki nilijikuta nakutana shamba zuri la migomba ,lakini kilichonivuta zaidi mpaka kuwa na shauku ya kusogea karibu ni uzio wa asili uliokuwa unazunguka shamba hilo,nilijikuta nataka nikaribie eneo hilo kwa karibu ili nionejinsi uzio huu ulivyotengenezwa kwa kutumia majamvi maarufu kama(ebilago au enshero)nikasogea kwa karibu zaidi,nilipofika getini nilichungulia kwa ndani ndo nikakutana na kitu kinaitwa hekaru lililojengwa migombani,nikazidi kusogea mafundi walikuwa wapo busy,nilimuhita mmoja wapo ili nijue mmliki wa bangaloo hilo,ndo nikaelezwa ni la profesa ANNA TIBAIJUKA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAKAZI.  SIKUSTUKA,kwa sababu nilianzia kufikiri enzi akiwa mwanaharakati,akapata wadhifa umoja wa mataifa UN HABITAT ,tena nafasi nyeti,katoka huko mojakwa moja kawa mbunge na hatimae waziri nikaona anastaili hekaru kama ili kuliweka migombani.
 Hata angekuwa wewe ungetamani kusogea karibu kujua kwenye uzio huu kuna nini.

 Sehemu ya mbele ya kuingilia,angalia geti la mbao linavyoendana na majamvi ya uzio
 Nikasogea taratibu nikakutana na kitu ,usipime na muleba migombani

 Kitu hicho cha profesa Anna Tibaijuka,ndo kinamaliziwa uwanja wa nje, ndani tayari kimeisha

 Sehemu ya juu, unaangalia chini,upepo mwanana na mandhali ya green usipime,muleba inatisha.


 Sehemu ya chini ya hekaru la profesa Anna Tibaijuka,lililopo muleba

 Kuna kitu cha msingi sana katika hekaru hili kuna njia ya walemavu wa viungo,wanasehemu yao ya kupita



 Jumba hili kwa hakika ni zuri na ni staili ya mama Anna Tibaijuka

 kwa mbele zimeanikwa kahawa,pamoja uaziri kilimo kinaendelea

           Pongezi sana mama Anna Tibaijuka, umejiandalia mazingira mazuri ya kuishi,wengi wao wangependa hekaru kama hili mtu analijenga mjini kwa maana ya biashara au kuishi,wewe umelijenga kagera,tena muleba migombani.ongera mama.                                                                                     

No comments:

Post a Comment