Sunday 3 August 2014

MIEMBENI FC MABINGWA WAPYA KAGASHEKI CUP 2014, WAIFUNGA TIMU YA KITENDAGURO FC BAO 2-1

Wachezaji wa Miembeni Fc wakifurahia na Mwali wao baada ya Kuwafunga bao 2-1 Makhirikhiri, Kitendaguro Fc leo jioni. Timu ya Miembeni ndio imeitwaa kombe hili kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 5.
TIMU ya Kata ya Miembeni Mitaa ya Uzunguni Bukoba leo hii imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa michuano ya kuwania Kombe la Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini KAGASHEKI CUP 2014 kwa mara ya kwanza baada ya kuinyamazisha Makirikiri wana wa Kitendaguro kwa kuilaza Mabao 2-1 katika mpambano ulioonekana mkali kwa Mashabiki wengi waliojitokeza katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.
Kipindi cha kwanza timu zote zilitoka bila kufungana katika dakika 45 za kipindi hicho, Kipindi cha pili dakika ya 56 Miembeni Fc walifanya mashambulizi hatari na kuliandama lango la wapinzani wao na kupata bao kupitia kwa mchezaji wake Babu Seif na baadae katika dakika ya 58 mchezaji huyo huyo Seif akawatungua bao la pili na kufanya Timu ya miembeni kuongoza kwa bao 2-0 dhidi ya Kitendaguro Fc wanaojulikana kwa jina la Makhirikhiri zaidi hapa Bukoba.

Dakika ya 67 Mchezaji wa Kitendaguro alifanikiwa kupata bao kupitia kwa Kassongo James na kubadilisha mchezo kuwa 2-1 na mtanange huo kumalizika kwa Timu ya Miembeni kuwa na Ushindi na kutwaa Kombe hilo la Ligi ya Kagasheki kwa huu 2014.
Timu ya Kitendaguro imekuwa ya pili na mshindi wa Tatu na waliokuwa Mabingwa watetezi Bilele Fc.

Kwa Upande wa Zawadi Mshindi wa kwanza ambaye ni Bingwa mpya Miembeni Fc amejishindia zawadi ya pesa Million tano, wa pili ambaye ni Kitendaguro wamepata Million tatu na watatu ambaye ni Bilele fc wamejipatia Tsh Million 1 na nusu.
Mapema mdhamini wa Ligi hii Kagasheki akisalimiana na Waamuzi wa MtanangeKikosi cha Miembeni Fc na Kocha wao Msaidizi Bw. Mwinyi Kikosi cha Kitendaguro Fc kilichoanza.Picha ya pamoja waamuzi na mqnqhodha wa Timu zote mbili.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa Mtanange wa Fainali kati ya Miembeni Fc na Kitendaguro Fc
Mchezaji wa Miembeni Fc akiwa kawekwa kati na wachezaji wa Kitendaguro FcMashabiki wa Timu ya Kitendaguro Fc wakiipamba timu yaoWachezaji wa Miembeni wakimpongeza Straika wao kwa kuwafungia bao la kwanza na kufanya 1-0 dhidi ya Kitendaguro katika dakika ya 56Wakishangilia tena dakika ya 58 baada ya  Babu Seif kuwapachikia bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya wenzao Kitendaguro Fc

Hapa ni baada ya dakika 90 kumalizika timu ya Miembeni Fc wakiwa mabingwa wapya wakishangilia ubinwa huo wa mwaka huu 2014 jioni ya leo mbele ya Umati mkubwa wa Watu waliojitokeza kuzishangilia timu hizo mbili na mbele ya Mdhamini Mkuu wa Ligi hiyo Mbunge wa Bukoba Mjini Khamis Sued Kagasheki.

Mdhamini Mkuu Mh. Khamis Sued Kagasheki akijichukulia picha za kumbukumbu uwanjani baada ya timu hizo kumaliza mtanange na timu ya Miembeni kuibuka na Ubingwa leo wa bao 2-1 dhidi ya timu ya Kitendaguro maarufu kama Makhirikhiri.Ukodaki time! Siku nyingi hatujaonana!! Ni Mdau Mc Baraka Galiatano na Msanii wa Bongo wa Filamu kali kali na yeye alikuja kushuhudia Fainali.Wachezaji wakivishwa Medali zaoKocha Mkuu wa Timu ya Miembeni Fc, Salum Bonge akiteta jambo na Mh. Khamis Kagasheki wakati wa zoezi la kupewa zawadi likiendelea.. Wachezaji wa Miembeni Fc ambao ndio Mabingwa wapya 2014 wakishangilia baada ya kupewa Kombe"Sisi ni ni Mabingwa 2014 Kagasheki Cup"Kiongozi Kocha Msaidizi wa Timu ya Miembeni Fc Mwinyi (kushoto) nae amepata muda wa kupata Ukodak na Mwali wao.

Umati wa Watu ulikusanyika kusikiliza neno kutoka kwa Mdhamini wa Ligi hii ya Kagasheki leo
Mbunge wa Bukoba Mjini Mh. Khamis Sued Kagasheki akiongea na Umati wa Watu kuhusu Ligi na Maendeleo yake leo hii kwenye Tamati ya Michuano hiyo ambayo leo hii ndio imehitimisha Mashindano ya Raundi ya Tano na ikiwa ni Mwaka wa tano mfululizo.Watu wakakubali swala la kuhusu kuboresha Ligi hiyo.Pia Mdhamini Mkuu Mh. Kagasheki ameongea na Wananchi hao kutoka katika kata zote 14 waliobahatika kuja hapo uwanjani kuwa Mwaka Kesho kutakuwepo na haja ya kuboresha Michuano hii.Mamia ya Watu walijitokeza kuona fainali ambayo ilizikutanisha timu ya Miembeni Fc na KITENDAGURO FC.Zawadi zilitolewa pia huyu ni Mchezaji kajipatia pesa taslim na BaiskeliKagasheki Cup.....oyeeee!!!!Zawadi zikaendelea kutolewa kwa Viongozi wa timu mbalimbali za Kata 14 zinazoshiriki Ligi hiiKitita cha pesa!Wachezaji wa Miembeni Fc wakijivinjali na Mwali waoWaliondoka na Mwali wao, Barabara ikafungwa kwa muda

No comments:

Post a Comment