Sunday 29 June 2014

KAGASHEKI CUP 2014: KASHAI 3 vs BAKOBA 0, MAJANGA!! MAHASIMU BAKOBA HOI KWA WENZAO, WAKUBALI YAISHE!! MASHABIKI WANUNA KAITABA!

Na Faustine Ruta, Bukoba
Michuano ya Kagasheki Cup 2014 imeendelea tena leo kwenye Uwanja wa Kaitaba ulipo Bukoba Mjini kwa siku ya pili na kushuhudia mahasimu wawili Mmoja akimliza mwenzake bao 3-0.
Mtanange wa leo hii Jumapili ulizikutanisha timu mbili matata kwenye hii ligi za Kashai na Bakoba FC na kushuhudia Timu ya Bakoba ikifungwa bao 3-0 bao zilizofungwa kipindi cha kwanza mbili na kipindi cha pili moja.
Timu ya Kashai FC walianza kuifunga timu ya Bakoba bao la kwanza katika dakika ya 8 bao likifungwa na Joha Johansen. 
Bao la pili lilifungwa na Msengi Gerard katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Bakoba FC ambao mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa hawajapata kitu.
Kipindi cha pili licha ya timu zote mbili kukamiana kwa sana timu ya Bakoba ilipata nafasi kama tatu lakini haikuweza kuifunga timu ya Kashai na hatimaye Kashai kupata bao lao la tatu katika dakika ya 60 kipindi cha pili bao lililotiwa nyavuni na Mchezaji wa Kashai FC Shamte Odilo na Kipute kumalizika kwa dakika 90 Kashai ikiibuka kwa bao 3-0. 
Michuano hii itaendelea tena kesho Jumatatu na kutakuwa na Mitanange miwili wakwanza utachezwa saa nane kati ya Nshambya FC ikiumana na timu ya Kibeta Fc saa 8:00 mchana na mtanange wa saa 10:00 ni baina ya Kagondo Fc na Buhembe Fc.

Mchezaji wa Shamte wa Timu ya Kashai akishangilia bao lake

Shamte na Joha Johansen wakishangilia bao
Tumu kapteni na Waamuzi katika picha ya PamojaMashabiki wa timu ya Bakoba wakiwa awaamini macho yao, timu ikipigwa bao la pili katika dakika ya 38Mashabiki wa Kashai Fc usipime!!Chinja!! Chinja!!! Mashabiki wa Kashai wakiipamba timu yao ili iendelee kutoa dozi kwa maasimu wao!Kipute kikiendelea...Mchezaji wa Bakoba akikimbia na mpira kwenda kufunga...Patashika wachezaji wakichuana kugombea mpiraMchezaji wa Kashi Fc akimbana mwenzake wa BakobaJukwaa kuu mashabiki wa Bakoba, hawana hamu!!! wengi mikono kichwani!! na wengine wakijiuliza kunani?? Na hapa ilikuwa na mapumziko Bakoba walienda kupumzika wakiwa nyuma ya bao 2-0.Kwa wengine mambo safi!Vijana wakitokelezea kwenye Camera Mwanadada Shabiki wa timu ya KashaiKipute kikiendelea...Vijana wa Kashai wakiwabana wenzao Bakoba Fc ili wasiweze kurudisha hata bao mojaMabeki wa kulia na kushoto wa timu ya Kashai wakimbana mchezaji mmoja wa BakobaPamoja sana!!Wazee nao hawakukosa!Mama Shabiki wa Bakoba Fc akiwa hana ili wa lile!! leo kakamatika!

Dakika 90 zimemalizika...Kashai 3 vs Bakoba 0
Mashabiki wakiondoka kwenye lango kuu la Uwanja wa Kaitaba!! Wengi wakijiuliza kwa nini timu moja imekubali yaishe hivi hivi!!! Tatizo ni nini??? Usajili au?

No comments:

Post a Comment